Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 20:51

Kuhusu sisi

Kuhusu sisi

Sauti ya Amerika (VOA) ni taasisi kubwa yenye aina mbalimbali za majukwaa ya matangazo ya habari za kimataifa, inayoandaa maudhui katika lugha zaidi ya 45 kwa wasikilizaji wenye kukabiliwa na ufinyu wa kupata habari au hawana njia ya kupata habari kutoka vyombo vilivyo huru.

Tangu ilipoanzishwa mwaka 1942, VOA imejizatiti kutoa matangazo kamilifu, huru na kuwaeleza wasikilizaji wake ukweli. VOA inafadhiliwa kikamilifu na walipa kodi wa Marekani ikiwa ni sehemu ya Taasisi ya Habari ya Kimataifa ya Marekani (USAGM).

Jukumu la VOA na uhuru wa habari uliowekwa na sheria inayowalinda waandishi wa habari wa VOA dhidi ya ushawishi, shinikizo, au kulipiziwa kisasi kunakoweza kufanywa na maafisa wa serikali au wanasiasa.

Mwaka 1976, Rais Gerald R. Ford alisaini Mkataba wa VOA, unaoeleza kuwa :

1. VOA itajishughulisha bila ya kusita kuendelea kuwa ni chanzo cha habari chenye kutegemewa na kuaminika. Habari zinazotolewa na VOA zitakuwa sahihi, zisizo na upendeleo na kamili.

2. VOA itaiwakilisha Marekani, na siyo kikundi kimoja cha jamii ya Marekani, na hivyo kutoa muelekeo wenye uwiano na ukamilifu wa fikra muhimu za Marekani na taasisi zake.

3. VOA itatoa sera za Marekani kwa ufasaha na ubora wake, na itaandaa mijadala makini na maoni juu ya sera hizi.

Mnamo mwaka 1994, Bunge la Marekani lilipitisha Sheria ya matangazo ya kimataifa ya Marekani. Sheria hii pia inataka kazi za waandishi wa habari ziwe za kuaminika, sahihi, zisizo kandamiza upande wowote.

Mwaka 2016, Bunge la Marekani kwa mara nyengine liliingiza katika sheria ya kuidhinisha Ulinzi wa Taifa kuwa ukusanyaji wa habari na majukumu ya kupasha habari lazima yaendelee kuwa huru na yasiyokandamiza upande wowote.

Kila siku, waandishi wa VOA wanafanya kazi kwa bidii kuweka mfano bora wa misingi ya uhuru wa habari ulimwenguni.

VOA

Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika ilikuwa Idhaa ya kwanza ya lugha ya Kiafrika kuanzisha matangazo kupitia mitambo ya Sauti ya Amerika mjini Washington D.C. Mwezi Mei 1962 matangazo ya dakika thelathini ambayo yalikuwa yamerekodiwa kwenye ukanda. Kuanzia mwaka 1962, yaligeuzwa na kufanywa kipindi kilichotangazwa moja kwa moja, kila siku kutoka Washington, kikirudiwa na kuongezewa habari mpya, mara moja kwa siku.

Mwezi Mei 1966, matangazo hayo yaliongezewa dakika nyingine thelathini na kuwa matangazo ya saa moja kukiwemo muziki uliorekodiwa na vipindi mbalimbali kutokea mjini Monrovia, Liberia. Na mwaka uliofuata, 1967, Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika ilizindua matangazo ya moja kwa moja kutoka studio zetu hapa Washington D.C. Leo, Idhaa ya Kiswahili imo hewani kwa muda wa saa 9 na nusu kwa wiki.

Matangazo ya Idhaa ya Kiswahili huwafikia mamilioni ya wasikilizaji katika Afrika Mashariki na eneo la Maziwa Makuu. Kiswahili ni lugha rasmi katika nchi za Afrika mashariki na ni lugha inayopanuka nchini Congo, Rwanda na Burundi. Kiswahili vile vile ni lugha inayozungumzwa na kueleweka katika eneo la kusini mwa Somalia, Visiwa vya Comoro na sehemu za kaskazini mwa Msumbiji na Malawi.

Kadhalika tuna idadi kubwa ya wasikilizaji katika nchi za Mashariki ya kati na kusini mwa Afrika.

Idhaa ya Kiswahili imepanua usikilizaji katika masafa ya FM kwa ushirikiano na redio nchini Kenya, Tanzania, Uganda na Rwanda na Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo.

MITA BENDI NA FRIKWENSI

Jumatutu hadi Ijumaa

1630-1700 UTC 15265 15460 17530

XS
SM
MD
LG