Tunatumia 'cookies' ili kuboresha huduma zetu kwako. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana katika sera yetu ya faragha.
Watu 17 wameuwawa Burundi na wengine 13 kujeruhiwa katika mashambulizi ya kuvizia dhidi ya magari 2 ya abiria mkoani Gitega. Waliohusika hawajatambulika. Hata hivyo, inashukiwa kuwepo kwa kundi linalofanya mashambulizi kama hayo, hii ikiwa ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja kwa watu kuuawa. Amida ISSA anaripoti kutoka Bujumbura.
Serikali ya mpito ya Sudan inakabiliwa na kizingiti katika hatua ya kukijumuisha jeshini kikosi maalum cha mgambo chenye nguvu nchini humo.
Mji wa Beni huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umewekwa chini ya sheria ya kuzuia watu kutoka nje baada ya kutokea mashambulizi matatu ya mabomu katika mji huo wa mashariki.
Shirika la mpango wa chakula duniani WFP laonya hali inatisha Kusini mwa Madagascar ambako maelfu wako kwenye hali ya njaa na maelfu wengine wako hatarini kutumbukia katika baa kubwa la njaa
Asasi za kiraia nchini Liberia zawasilisha rasimu ya sheria bungeni ili kuundwa korti ya uhalifu nchini humo miaka 20 baada ya vita vya wenyenye kwa wenyewe.
Yaliyoandikwa kwenye magazeti ya Ujerumani juu ya Afrika ni pamoja na baa la njaa kwenye jimbo la Tigray, juu ya kuaga dunia kwa mwasisi wa taifa huru la Zambia, Dr.Kenneth Kaunda miongoni mwa mengine.
Museveni azishutumu nchi za magharibi kwa kuhodhi chanjo
Hali ya usalama inazidi kuzorota katika mji wa Beni, ambako kuna taarifa za kutegwa mabomu ya kutengenezwa kienyeji katika maeneo na majengo mbalimbali yakiwemo makanisa. Ndani ya kipindi cha masaa 48 yaliyopita siku ya Jumamosi (26.06.2021), mabomu matatu yaliripuka na kusababisha kifo cha mtu mmoja pamoja na majeruhi kadhaa. John Kanyunyu anaripoti kutoka Beni.
Afrika inakabiliwa na wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona, wakati hospitali zikiendelea kuwapokea wagonjwa na vifo vikishuhudiwa hali ambayo imechangia vituo vya afya kulemewa.
Matamshi ya jenerali Elly Tumwine kumtaka rais Museveni ajiandae kung’atuka yamepokelewa kwa maoni ya mshangao na mshtuko kwani anafahamika kuwa mfuasi wake mwaminifu na wa jadi katika historia ya mapambano yao miaka ya themanini. Isikilize ripoti ya mwandishi wa DW aliyeko Kampala, Uganda, Emmanuel Lubega.