Tunatumia 'cookies' ili kuboresha huduma zetu kwako. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana katika sera yetu ya faragha.
Tanzania: Katika kuadhimisha siku zake 100 madarakani, Rais amekutana na wahariri wa vyombo vya habari na waandishi / Mbeya: Mahakama imemuachia huru Mdude Nyangali/ Je, Afrika tuna miundo mbinu na ujuzi wa kutosha wa kutengeneza chanjo dhidi ya COVID-19?/ UN: Ubaguzi wa rangi dhidi ya waafrika ni wa kimfumo duniani/ Kongo: imetangaza kupunguzwa bei ya nauli ya ndege na za baadhi ya vyakula Nenda kwenye sauti
Uganda: Museveni ameyakosoa mataifa ya Magharibi kwa kile anachokitaja kuhodhi chanjo za COVID-19 dhidi ya mataifa yanayoendelea hasa bara Afrika/ Burundi: Watu 17 wameuwawa na wengine 13 kujeruhiwa katika mashambulizi/ Hali ya usalama inazidi kuzorota katika mji wa Beni/ Iraq, Misri na Jordan zafanya mkutano wa kilele Nenda kwenye sauti
Watu 17 wameuwawa Burundi na wengine 13 kujeruhiwa katika mashambulizi ya kuvizia dhidi ya magari 2 ya abiria mkoani Gitega. Waliohusika hawajatambulika. Hata hivyo, inashukiwa kuwepo kwa kundi linalofanya mashambulizi kama hayo, hii ikiwa ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja kwa watu kuuawa. Amida ISSA anaripoti kutoka Bujumbura. Nenda kwenye sauti
Hali ya usalama inazidi kuzorota katika mji wa Beni, ambako kuna taarifa za kutegwa mabomu ya kutengenezwa kienyeji katika maeneo na majengo mbalimbali yakiwemo makanisa. Ndani ya kipindi cha masaa 48 yaliyopita siku ya Jumamosi (26.06.2021), mabomu matatu yaliripuka na kusababisha kifo cha mtu mmoja pamoja na majeruhi kadhaa. John Kanyunyu anaripoti kutoka Beni.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameyakosoa mataifa ya Magharibi kwa kile anachokitaja kuhodhi chanjo za COVID-19 dhidi ya mataifa yanayoendelea hasa bara Afrika. Museveni ameyahimiza mataifa ya Afrika kujishughulikia yenyewe kwa masuala ya chanjo, huku akifichuwa kuwa Uganda itakuwa na chanjo yake ya COVID-19 kufikia mwishoni wa mwaka huu. Lubega Emmanuel anaripoti.
Mto wa Nairobi umechafuka. Hata hivyo vijana wa eneo la Kibra ambako mto huo unapitia wameamua kuusafisha ili kuunusuru. Juhudi zao zimetambulika baada ya mmoja wao kwa ushirikiano na wenzake kutunukiwa tuzo ya mwanamuziki bora zaidi. Makala ya mazingira inaangazia juhudi za vijana wa Kibra kuusafisha Mto Nairobi.
Katika Sura ya Ujerumani, safari hii tunaangazia kwa nini vuguvugu la vijana wa mashariki ya Ujerumani wanakiunga mkono chama cha Mbadala kwa Ujerumani, AfD.
Shirika la Uangalizi wa Haki za Binaadamu la nchini Syria, lenye maskani yake mjini London, Uingereza limesema mashambulizi ya anga ya Marekani katika eneo la mpakani mwa Syria na Iraq yamewauwa wanamgambo watano.
Wakili wa mshambuliaji wa Wuerzburg anasema huenda mteja wake akajidhuru. Maelfu ya wafanyakazi wahamiaji wakimbia Bangladesh kukwepa vizuizi vya Corona. Rais wa Misri Abdul Fattah Al-Sisi azuru Iraq kwa mara ya kwanza.
Kirusi cha Delta chalazimisha vizuizi vipya vya kudhibiti kuenea kwa corona. Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aukosoa utawala wa rais Joe Biden. Watu 2 wajeruhiwa katika shambulizi la bomu kanisani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Waziri wa Afya wa Uingereza ajiuzulu kwa kukiuka kanuni za Corona// Waandishi wa habari washambuliwa kwenye maandamano Argentina// Italia yajiunga na Denmark katika robo fainali Euro 2020
Maelfu ya Wapalestina wamefanya maandamano mengine leo kufuatia kifo cha mkosoaji wa serikali. Polisi ya Ujerumani imeanzisha uchunguzi kuhusu shambulio la kisu la mjini Wuerzburg. Mamia kwa maelfu ya watu wanakabiliwa na baa la njaa nchini Ethiopia.
Kansela wa Ujerumani amesema misimamo ya Hungary ni kitisho kwa hatma ya Umoja wa Ulaya. Rais Joe Biden amesema Marekani itaendelea kuiunga mkono Afghanistan. Rais wa Msumbiji ameapa kuwatokomeza kuwatokomeza wanamgambo wa itikadi kali.
Ametazama akang'amua kuwa tuzo zimekuwa zikitolewa kwa watu waliotia fora katika tasnia mbali mbali, lakini kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa na pia makampuni, hakuna tuzo iliyopo kutambua juhudi zao. Ni Diyana Laizer, ambaye stori yake ya kuanzisha Consumers Award anakuletea Hadija Halifa. #MsichanaJasiri 25.06.2021
Tanzania: Siku 100 tangu Rais wao Samia Suluhu Hassan aingie madarakani/ Liberia wataka kuundwa korti ya uhalifu nchini humo/ Mwanaharakati wa haki za binadamu Palestina Nizar Banat afariki/ Rais Joe Biden akutana na Ashraf Ghani wa Afghanistan/ Kenya; Tejveer Rai,dereva wa mbio za magari, asafirishwa kupokea matibabu/ Aliyekuwa mchambuzi DW Padri Privatus Karugendo afariki dunia
Mahakama Kuu imebatilisha hukumu ya Hakimu mkazi Kisutu/ Umoja wa Ulaya umelikataa pendekezo la Ujerumani na Ufaransa lililoutaka Umoja huo kurejesha utaratibu wa mikutano na Rais Vladimir Putin wa Urusi /Wimbi la maambukizi ya kirusi cha Corona limerudi tena kwa kasi barani Afrika/Makaburi 751 yagunduliwa nchini Canada karibu na shule ya watoto wa kiasili