Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:48

Kundi mshirika wa Al Qaeda ladai kuua mamluki 4 wa Russia nchini Mali


Waandamanaji nchini Mali wakishilikia bango linalosomeka " asante Wagner", jina la kampuni ya ulinzi ya kibinafasi ya Russia iliyopo nchini Mali. Picha ya AFP
Waandamanaji nchini Mali wakishilikia bango linalosomeka " asante Wagner", jina la kampuni ya ulinzi ya kibinafasi ya Russia iliyopo nchini Mali. Picha ya AFP

Kundi mshirika wa Al Qaeda nchini Mali Jumatatu limedai kuwaua mamluki wanne wa kundi la Russia la Wagner katika shambulio la kuvizia karibu na eneo la Bundiagara katikati mwa Mali.

Kitengo cha habari cha kundi la Jama’ at Nursat al-Islam wal Muslimeen (NIM), kimesema katika taarifa kwamba wapiganaji wa kundi hilo walipambana na mamluki hao Jumamosi katika jimbo la Mopti, kulingana na tafsiri ya tovuti ya kundi la ujasusi, ambalo linafuatia taarifa za kundi hilo la wanamgambo wa kiislamu.

Wagner haina mwakilishi wa kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na haikuweza kupatikana ili kutoa maelezo.

Mali inatatizika kukomesha uasi wa wanamgambo wa Kiislamu uliokita mizizi baada ya ghasia za 2012 na kuenea tangu wakati huo katika nchi jirani, na kuua maelfu ya watu na kulazimisha mamilioni ya wengine kuhama makazi yao katika eneo la Sahel la Afrika magharibi.

Wagner ilianza kupeleka mamia ya wapiganaji mwaka jana kuunga mkono jeshi la Mali na imeshtumiwa tangu wakati huo na makundi ya haki za binadamu na wakazi kwa kushiriki katika mauaji ya raia, na kundi hilo halijatoa maelezo juu ya tuhuma hizo.

Serikali ya Russia ilikiri kwamba kuna wafanyakazi wa Wagner ambao wako nchini Mali lakini serikali ya Mali iliwaelezea kama wakufunzi kutoka jeshi la Russia badala ya makandarasi wa usalama wa kibinafsi.

XS
SM
MD
LG