Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:06

Surua yaendelea kusambaa Zimbabwe


Wazai wapanga foleni ili kupata chanjo za Surua kwa watoto wao
Wazai wapanga foleni ili kupata chanjo za Surua kwa watoto wao

Zimbabwe imesema Jumanne kwamba mlipuko wa Surua nchini humo kufikia sasa umeua takriban watoto 157, huku kukiwa na zaidi ya maambukizi 2,000 yaliyoripotiwa kote nchini.

Kesi za maambukizi zimekuwa zikiongezeka kwa haraka kwenye taifa hilo la Afrika kusini tangu kutangazwa rasmi kwa kesi ya kwanza mapema mwezi huu, wakati idadi ya vifo ikisemekana kuongezeka maradufu ndani ya muda wa chini ya wiki moja. Waziri wa afya Monica Mutsvangwa wakati akizungumza mbele ya wanahabari baada ya kumaliza kikao cha kila wiki cha baraza la mawaziri, amesema kwamba kufikia Jumanne kesi za maambukizi kote nchini zilikuwa 2,056 na vifo 157.

Mutsvangwa amesema kwamba serikali itaongeza juhudi za utoaji chanjo pamoja na kutumia sheria ya muda itakayoiruhusu kutumia fedha kutoka mfuko wa kitaifa wa dharura, ili kukabiliana na janga hilo. Ameongeza kusema kwamba serikali itashauriana na viongozi wa kimila na kidini kwenye kampeni hiyo, ili kutoa uhamasisho, kwa kuwa wengi walioambukizwa au kufa hawajawahi kupewa chanjo. Hapo awali wizara ya afya ililaumu mikusanyiko ya kidini kwa kueneza maabukizi hayo kwa haraka.

XS
SM
MD
LG