Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 11:14

Waandishi na watetezi waonya kuhusu vitisho kwa uhuru wa habari kupitia teknolojia


Watu wakishiriki kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani. May 3, 2012.
Watu wakishiriki kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani. May 3, 2012.

Katika maadhimisho ya siku ya  Uhuru wa Habari Duniani, waandishi na watetezi wa haki za binadamu wameonya kuhusu vitisho kwa uhuru wa habari na demokrasia kwa kutoa habari za uongo, hotuba za chuki na propaganda  kupitia teknolojia ya digitali.

Katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Habari Duniani, waandishi na watetezi wa haki za binadamu wameonya kuhusu vitisho kwa uhuru wa habari na demokrasia kwa kutoa habari za uongo, hotuba za chuki na propaganda kupitia teknolojia ya digitali.

Katika tukio maalum kuadhimisha siku hiyo , mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet alitoa heshima kwa ushujaa na azma ya waandishi wa habari ambao wanaendelea kufanya kazi huku wakikabiliwa na ongezeko la manyanyaso, vitisho, na hatari kwa maisha yao.

Bachelet alielezea kuwa mwaka jana waandishi wa habari 55 waliuwawa. Mwaka huu, anasema waandishi wa habari sita na mfanyakazi mmoja kwenye chombo cha habari aliuliwa huko Mexico na waandishi wa habari wengine 12 wameuawa nchini Ukraine tangu Russia ilipoivamia nchi hiyo hapo Februari 24 ameonya kuhusu ongezeko la nyenzo za upelelezi, kama vile Pegasus au Candiru, ambavyo vinaingilia kwa ndani vifaa vya watu na maisha yao.

“Matumizi ya udukuzi katika mitandao umepelekea kukamatwa, kutishiwa na hata kuuawa kwa waandishi wa habari. Imehatarisha vyanzo vyao. Inaziweka hata familia zao katika hatari. Kukabiliana na hatari hizi, waandishi wa habari mara nyingi wanachukua njia hatari za kujizuia.”

Mshindi wa tuzo ya mwaka ya Amani ya Nobel, mwandishi wa habari wa Russia, Dmitry Muratov, anasema Russia inakabiliwa na mustakbali uliovunjika kwasababu ya Rais Vladimir Putin. Anasema uharibifu wa vyombo huru chini ya utawala wa Putin, na propaganda dhidi ya Ukraine, zimekuwa ni muhimu katika kuchochea uvamizi wa Russia.

Mshindi mwenza wa tuzo hiyo mwaka jana, mwandishi wa habari wa Ufilipino, Maria Ressa anakiri kuhusu ukandamizaji wa ukweli uliofanywa na Putin ambapo imewezekana kwake kuanzisha vita nchini Ukraine.

“Bila ya takwimu huwezi kupata ukweli. Bila ya ukweli huwezi kupata uaminifu. Bila ya uaminifu hatushirikiani uhalisia. Hakuna kanuni za sheria. Hakuna demokrasia. Waandishi wa habari, watetezi wa haki za binadamu – mtu yeyote anashambuliwa, mtu yeyote anaweza kulengwa. Sisi hatuna ulinzi katika vita vya habari,” anasema Ressa.

Ressa anasema propaganda inakuwa na mchango katika kuwatia khofu watu na kuwasilisha takwimu za uongo. Anaonya kuwa watu ambao wanaamini uongo ndiyo sahihi, ni watu ambao wanaweza kudhibitiwa. Anaonya pale ukweli unapoharibiwa, demokrasia nayo huharibiwa.

XS
SM
MD
LG