Radio
06:00 - 06:29
Masuali yaibua baada ya wanajeshi wa Burundi kuingia rasmi DRC
Wakazi wa mkoa wa Kivu Kusini wanajiuliza kipi kitafuata baada kikosi cha wanajeshi wa Burundi kuruhusiwa kuingia kwenye ardhi ya Congo mapema wiki hii, chini ya mpango wa Jumuia ya Afrika mashariki kupambana na makundi ya kigeni yenye silaha mashariki mwa DRC.
16:30 - 16:59
Mikataba ya wasanii yaendelea kukumbwa na changamoto
Wasanii wanaoingia katika mikataba mbalimbali na makampuni ya promotion wamejipata katika njia panda baada ya kugundua kwamba hawakusoma maudhui ya mikataba hiyo kwa makini, na wanashauriwa kuwa makini zaidi kabla ya kujiingiza katika hali wasiyoweza kudhibiti.
21:00 - 21:29
Kwa Undani: Donald Trump aonyesha ubabe wa kisiasa katika chama cha Republican, Ruto ajitayarisha kuunda serikali Kenya
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.