Wadau wa elimu nchini Kenya wameshtumu agizo la serikali la ghafla la kuamrisha kufungwa kwa shule zote nchini humo baada ya wiki tatu tu shule kufunguliwa kufuatia kukamilika kwa muhula wa masomo.
Mchuano ni mkali katika uchaguzi wa rais na wabunge nchini Kenya. Vijana wapewa wito wa kuzingatia amani na utulivu, hasa wakati na baada ya uchaguzi. Na mchambuzi Jackline Adhiambo anasema vijana wameonyesha ukomavu.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.