Radio
06:00 - 06:30
Raia wa Burundi walalamikia uhaba wa mafuta ya petroli
Wakati serikali ya Burundi ikikiri kwamba imeleta mafuta ya kutosha ya petroli kutoka katika nchi za kigeni ili kukabiliana na uhaba wa bidhaa hiyo, raia wanalalamika kwamba mafuta hayo yanaendelea kukosekana katika maeneo ya mikoani ambapo nauli ya usafiri imepanda kwa kiasi kikubwa.
19:30 - 19:59
21:00 - 21:29
Angola: Upinzani waelekea mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu
Chama kikuu cha Upinzani cha Angola, UNITA, kimeliambia shirika la habari la AFP kwamba kitapinga matokeo ya uchaguzi mahakamani baada ya tume ya uchaguzi kutangaza chama cha rais aliye mamlakani kama kilichoshinda uchaguzi wa wiki jana kwa asili mia 51 ya kura.