Radio
Kenya: Mahakama ya Juu yatupilia mbali ombi la Ruto la kupinga kushtakiwa kwa maafisa 6 wa IEBC
Hatua ya Rais mteule wa Kenya William Ruto kuitaka Mahakama ya Juu kuwazuia makamishna sita wa tume ya uchaguzi kushtakiwa katika kesi ya kupinga ushindi wake akidai kuwa IEBC inafanya kazi kama tume lakini si ya makamishna binafsi imetupiliwa mbali.
Kesi ya Uchaguzi wa Rais yaendelea katika Mahakama ya Juu Kenya
Mawakili wanaomwakilisha Raila Odinga katika kesi ya kupinga uchaguzi wamesema kuwa uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022 ulitokana na hila za IEBC na Rais mteule William Ruto. Kulingana na Wakili Mkuu James Orengo, mahakama hiyo iliwaruhusu kutazama seva yake moja tu kati ya nane.
Maoni mseto baada ya serikali ya Kenya kuzindua mfumo mpya wa namba za Magari
Baada ya serikali ya Kenya kutangaza kwamba wenye magari ni sharti wapate na kuweka vibandiko vipya vya kidijitali kwenye magari yao, maoni mseto yanaendelea kutolewa huku baadhi wakisema hatua hiyo haina umuhimu wowote huku nayo serikali ikitetea mpango huo kama njia ya kuzuia au kudhibiti uhalifu.