Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook
Pata taarifa kuu

Hamas kushiriki mazungumzo mapya kujaribu kupata makubaliano na Israel ya kusitisha vita Gaza

Ujumbe wa kundi la Hamas, unatarajiwa kwenda jijini Cairo kwa ajili ya mazungumzo mapya kujaribu kupata mwafaka na Israeli, kusitisha vita vinavyoendelea kwenye ukanda wa Gaza.

Khalil al-Hayya, kiongozi wa juu wa Hamas.
Khalil al-Hayya, kiongozi wa juu wa Hamas. AP - Khalil Hamra
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa juu wa kundi la Hamas Khalil al-Hayya amesema, atawasilisha majibu kwa wasuluhishi wa vita hivyo, Qatar, Misri na Marekani kuhusu mapendekezo ya Israeli kuhusu usitishwaji wa vita vinavyoendelea.

Wakati mkutano huo, ukisubiriwa, rais wa Marekani Joe Biden, amezungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na kusisitiza msimamo wa nchi yake, kutounga mkono mpango wa Israeli kutuma vikosi vya ardhini kwenye mji wa Rafah.

Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas, ameiomba Marekani, kushawishi Israeli kuachana na mpango wake, anaosema iwapo utaendelea, utakuwa na madhara makubwa kwa Wapalestina.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya nje wa Markani Anthony Blinken anarejea tena nchini Saudi Arabia kuendeleza shinikizo za Israel na Hamas kusitisha vita, huku mwenzake wa Ufaransa Stéphane Séjourné anayezuru Lebanon, kujaribu kutafuta suluhu ya mzozo unaochipuka kati ya Israel na kundi la Hezbollah

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.