Nyota wa zamani wa Ligi ya Mpira wa Marekani NFL na mcheza filamu ambaye alifutiwa mashtaka ya mauaji ya mkewe na rafiki yake wa kiume katika kesi iliyoteka Marekani na dunia amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.
Jeshi la anga la Ukraine limesema ulinzi wa anga wa nchi hiyo ulitungua ndege 39 kati ya 40 zisizokuwa na rubani
Takribani kilo 608 za cocaine nyingi zikiwa katika mfumo wa maji zilikamatwa katika operesheni kwenye majimbo matatu
Walinzi wa pwani wamesema walipeleka boti yao ya doria katika eneo la tukio, ambapo iliwaokoa manusura 22
Hii inafuatia makundi ya kimataifa ya misaada ya kibinadamu kulalamika kuhusu vizuizi vilivyoko huko Gaza
Wakazi wa Marekani wanajiandaa kushuhudia tukio kubwa la kupatwa kwa jua Aprili Nane.
Katika mahojiano na VOA, kampeni ya Rais Joe Biden ya kutaka kuchaguliwa tena haikutilia maanani tukio moja la rekodi ya uchangishaji fedha lililofanyika Jumamosi na kampeni ya Donald Trump.
Waziri wa fedha wa Marekani, Janet Yellen, Jumapili amemwambia Waziri Mkuu wa China, Li Qiang, kuwa uwezekano wa kufanya mazungumzo magumu umeyaweka mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa sana kwenye msimamo thabiti zaidi katika kipindi cha mwaka uliopita.
Wapatanishi wa Marekani na Israel wanatarajiwa mjini Cairo mwishoni mwa juma hili kwa ajili ya msukumo mpya wa kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano katika vita ambavyo vimeendelea kwa karibu nusu mwaka.
Maafisa wanasema tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 4.7 vipimo vya rikta lilitikisa eneo la jiji lenye watu wengi la New York City. Wakazi waliripoti kuwa walihisi kunguruma kote kaskazini mashariki siku ya Ijumaa asubuhi.
Joe Biden na Donald Trump wameshinda uchaguzi wa awali katika vyama vyao kwenye jimbo la Magharibi kati la Wisconsin wiki hii, huku wote wakiwa na uhakika wa uteuzi.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani anasema Israel inahitaji hatua bora kuwalinda wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu na raia.
Pandisha zaidi