Wizara ya biashara ya Marekani Jumatatu imetoa mkopo wa dola bilioni 6.4 kwa kampuni ya elektroniki ya Samsung yenye makao yake Korea Kusini, ili kujenga kiwanda chake kipya cha kutengeneza chip za komputa mjini Taylor, Texas pamoja na kupanua kiwanda cha zamani mjini Austin kwenye jimbo hilo hilo.
Shirika lisilotafuta faida linasaidia wahamiaji kupata mafunzo kuhus ajira. Mafunzo haya hutolewa kuwaandaa wafanyakazi kufahamu masuala ya usalama katika viwanja vya ujenzi. Hii ni hatua ya kukabiliana na uhaba wa wafanyakazi wa ujenzi katika jiji la New York. Endelea kusikiliza...
Kesi ya kwanza ya uhalifu inayomkabili Rais wa zamani wa Marekani inatarajiwa kuanza wiki hii huko New York.
Israel, Jumapili imesema Iran ilifanya mashambulizi ya makombora 320 ya kivita dhidi yake katika shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa, lakini ulinzi wake wa anga pamoja na Marekani na nchi nyingine zinazoiunga mkono uliyatungua kwa asilimia 99.
Msemaji wa masuala ya usalama wa taifa wa White House, John Kirby, amesema Marekani na washirika wengine wanaona yalikuwa ni mafanikio ya makubwa ya kijeshi ya Israel, katika kuzima mashambulizi ya zaidi ya ndege zisizo na rubani 300 na makombora yaliyorushwa na Iran.
Donald Trump, anaelekea mahakamani Jumatatu, akiwa ni rais wa kwanza mstaafu wa Marekani kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu na tishio la kufungwa jela iwapo atapatikana na hatia.
Nyota wa zamani wa Ligi ya Mpira wa Marekani NFL na mcheza filamu ambaye alifutiwa mashtaka ya mauaji ya mkewe na rafiki yake wa kiume katika kesi iliyoteka Marekani na dunia amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.
Jeshi la anga la Ukraine limesema ulinzi wa anga wa nchi hiyo ulitungua ndege 39 kati ya 40 zisizokuwa na rubani
Takribani kilo 608 za cocaine nyingi zikiwa katika mfumo wa maji zilikamatwa katika operesheni kwenye majimbo matatu
Walinzi wa pwani wamesema walipeleka boti yao ya doria katika eneo la tukio, ambapo iliwaokoa manusura 22
Hii inafuatia makundi ya kimataifa ya misaada ya kibinadamu kulalamika kuhusu vizuizi vilivyoko huko Gaza
Wakazi wa Marekani wanajiandaa kushuhudia tukio kubwa la kupatwa kwa jua Aprili Nane.
Pandisha zaidi