Maafisa wanasema tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 4.7 vipimo vya rikta lilitikisa eneo la jiji lenye watu wengi la New York City. Wakazi waliripoti kuwa walihisi kunguruma kote kaskazini mashariki siku ya Ijumaa asubuhi.
Joe Biden na Donald Trump wameshinda uchaguzi wa awali katika vyama vyao kwenye jimbo la Magharibi kati la Wisconsin wiki hii, huku wote wakiwa na uhakika wa uteuzi.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani anasema Israel inahitaji hatua bora kuwalinda wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu na raia.
Uamuzi huo unafuatia mkutano wa baraza la mawaziri chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu wa Somalia Hamza Barre mjini Mogadishu.
Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen amewasili Guangzhou leo Alhamisi kuanzia ziara ya ufuatiliaji huko China ikiwa ni chini yam waka mmoja.
Blinken anaanza ziara yake mjini Paris, ambako wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema atakutana na Rais Emmanuel Macron
Ikinukuu chanzo cha usalama kisichojulikana, kituo hicho kilisema Ibrahim Dbeibah hakuwepo nyumbani wakati roketi hizo zilipopiga
Gavana wa mkoa wa Belgorod aliripoti uharibifu wa nyumba na umeme ikiwa ni matokeo ya vifusi
Jeshi la Israel limesema limewaua wanamgambo 200 katika eneo la hospitali hiyo ya Shifa
Walioshuhudia wanasema shambulizi la anga la Israel lilipiga mahema kadhaa ndani ya hospitali ya Al-Aqsa Martyrs
Hatua hii inafuatia shambulio baya zaidi kuwahi kutokea nchini humo ambapo watu wasiopungua 144 waliuawa.
Pandisha zaidi