Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, amepangiwa kuhojiwa na maafisa wa uangalizi wa New York, leo hii, hatua inayohitajika kabla ya hukumu yake ya Julai katika kesi yake ya uhalifu ya kulipa fedha za “kumnyamazisha mtu” kwa mujibu wa watu watatu wanaofahamu mpango huo.
Rais wa Marekani Joe Biden leo amekamilisha ziara yake ya Ufaransa kwa kutoa heshima zake kwenye makaburi ya wanajeshi wa Marekani, hatua ambayo rais wa zamani Donald Trump aliepuka wakati alipokuwa madarakani.
Mgombea Urais wa Marekani, Donald Trump anasema atakata rufaa kutokana na maamuzi ya kukutwa na hatia ya uhalifu kwa kugushi rekodi za biashara kabla ya uchaguzi wa 2016.
Jopo la mahakama wanajadili kesi ya uhalifu dhidi ya mgombea Urais wa Marekani, Donald Trump.
Mawakili wa mtoto wa kiume wa rais wa Marekani joe Biden, Hunter Biden Jumanne wanawasilisha hoja mahakamani, kwenye ufunguzi wa kesi ya uhalifu dhidi yake, ikitarajiwa kuhusisha ushahidi kutoka kwa wapenzi wake wa zamani na maelezo binafsi kuhusu matatizo yake ya matumizi ya dawa za kulevya.
Vyombo vya habari vya Marekani vimesema kuwa rais wa Marekani Joe Biden Jumanne atazindua amri ya kiutendaji ambayo itapunguza kwa idadi kubwa watu wanaoomba hifadhi kwenye mpaka wa Marekani na Mexico.
Saa chache baada ya kujiunga na mtandao wa kijamii wa TikTok, mgombea urais wa Repablikan Marekani Donald Trump, tayari amejipatia zaidi ya wafuasi milioni 1 kwenye jukwaa hilo alilojaribu kulipiga marufuku wakati alipokuwa rais, kwa misingi ya kulinda usalama wa taifa.
Uamuzi wa jopo la majaji wa New York kumtia hatiani rais wa zamani unaonyesha hakuna mtu aliye juu ya sheria, inasema kampeni ya Biden
Kama chama cha ANC kitashindwa itakuwa ni mara ya kwanza kupoteza viti vingi bungeni tangu kumalizika enzi ya ubaguzi wa rangi 1994.
Napenda kuwahakikishia kuwa Umoja wa Mataifa unasimama katika mshikamano na watu wa Iran, anasema Antonio Guterres
Jopo la wajumbe wa mahakama moja mjini New York, Alhamisi limempata na hatia rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kwa mashtaka 34 ya kugushi hati zake za biashara.
Tunaweza kuwa na miezi mingine saba ya mapigano ili kuimarisha mafanikio yetu na kuharibu nguvu za Hamas
Pandisha zaidi