Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 24, 2024 Local time: 15:42

Serikali ya Tanzania yasema wananchi walivamia eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)


Wafugaji wa kimasai katika eneo la ardhi karibu na uwanja wa ndege wa KIA
Wafugaji wa kimasai katika eneo la ardhi karibu na uwanja wa ndege wa KIA

Serikali ya Tanzania imetoa kauli kufuatia mgogoro wa Ardhi kati ya wananchi na serikali unaohusisha eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)

Mgogoro huo unaohusisha baadhi ya vijiji vya wilaya za Hai na Arumeru ambavyo vimeelezwa kuingia katika eneo la uwanja huo hali inayopelekea uharibifu wa mazingira katika eneo la uwanja na kupelekea ugumu katika utuaji wa ndege.

Baadhi ya wanavijiji wamesema wao sio wavamizi wa eneo hilo kwakuwa wamelimiliki kwa muda mrefu na serikali ilikuwa imekwishapeleka huduma za kijamii ikiwemo huduma za shule na maji.

"Vijiji hivyo vimesajiliwa kwa mujibu wa sheria vijiji vina shule vina barabara vina umeme vina maji kama sisi ni wvamizi kwanini hawataki kutushitaki kuthibitisha kwamba sisi ni wa vamizi anaibuka tu mkuu wa mkoa ambaye anakuja kuwaita watu wavamizi ambao wapo kwenye vijiji vyao halali kuna wazee wanazaidi ya miaka 70 wamezaliwa pale." alisema Ndasikoi.

Kwa mujibu wa Msemaji mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi ameeleza kuwa eneo hilo lilianza kumilikiwa na serikali kabla ya mwaka 1969 likijulikana kama pori Tengefu la Sanya Lelatema na ilipofika mwaka 1989 eneo hilo lilipimwa rasmi kwa ramani ya upimaji likiwa na hekta 11,085.

Matinyi ameongezea kuwa wananchi wamehamishwa katika eneo hilo ili kuhakikisha panakuwa na uendeshaji salama wa uwanja wa ndege, na shillingi billioni 11.3 zimetengwa kwa ajili ya kulipa fidia wananchi waliokwisha endeleza maeneo yao.

Hata hivyo kwa upande wa wananchi ambao wamekwisha kubali kuhama katika maeneo yao wameitaka serikali kupeleka huduma za kijamii katika maeneo waliyohamia ikiwa ni pamoja na shule, maji na umeme kama anavyoeleza Richard Molinge ambaye ni Mwenyekiti wa kijiji cha Tingiliani Wilayani Hai.

Matinyi amemalizia kuwa kufikia April 30, 2024 jumla ya wananchi 1,666 kati ya 1,712 walikwishalipwa malipo yao yenye thamani ya shillingi bilioni 11.2 na wamekwishaondoka katika makazi yao kwa hiari.

Forum

XS
SM
MD
LG