Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 28, 2024 Local time: 15:52

Kagame akubali kukutana na Tshisekedi kuzungumzia mzozo wa mashariki ya DRC


Kagame akubali kukutana na Tshisekedi kuzungumzia mzozo wa mashariki ya DRC
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:33 0:00

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Angola Tete Antonio amesema Jumatatu kwamba Rais Paul Kagame wa Rwanda amekubali kukutana na mwenzake wa Jamhiri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mazungumzo kuhusu hali ya usalama mkashariki ya Congo.

Antonio alizungumza na waandishi habari baada ya Rais Kagame kukutana na mwenyeji wake Joao Lourenco katika ikulu Lunda kwa mazungumzo juu ya ushirikiano kati ya nchi zao mbili.

"Wakati wa mkutano huo walikubaliana kwamba Rais Kagame ataweza kukutana na Rais Tshisekedi katika wakati utakaofikiwa na wapatanishi," amesema Antonio

Ofisi ya rais wa Rwanda kwenye ujumbe wake katika ukurasa wake wa X imeeleza kwamba wakuu hao wamekubali juu ya hatua muhimu kuelekea kutanzua sababu msingi wa ugomvi na haja ya kuheshimu utaratibu wa makubaliano ya Luanda na Nairobi wa kupatikana Amani na utulivu katika kanda nzima.

"Ujumbe wa Rwanda ulikubali kimsingi na ujumbe wa Congo kwamba mawaziri wao watafanya kazi pamoja ili kufikia lengo hilo," amesema Antonio.

Mwishoni mwa mwezi Februari, Antonio anasema Rais Tshisekedi kimsingi ameshakubali kukutana na mwezake wa Rwanda. Mara ya mwisho viongozi hao kukutana ilikua Februari 16 kando ya mkutano wa

viongozi wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa wakati wa mkutano mdogo wa kilele ulotayarishwa na Rais Lourenco.

Forum

XS
SM
MD
LG