Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 28, 2024 Local time: 19:31

Hatimaye suluhisho la mzozo kati ya wakulima na wafugaji lapatikana Nigeria


Rais wa Nigeria Bola Tinubu
Rais wa Nigeria Bola Tinubu

Kwa miaka kadhaa wadau wa kilimo nchini Nigeria wamekuwa wakitafuta suluhisho kwa mzozo kati ya wakulima na wafugaji.

Polisi jimbo la Kano wakiwaweka washukiwa wa wizi wa ng'ombe chini ya ulinzi katika kijiji cha Dajin Gomo village of Sumaila eneo la Kano, Nigeria, Novemba 2, 2015.
Polisi jimbo la Kano wakiwaweka washukiwa wa wizi wa ng'ombe chini ya ulinzi katika kijiji cha Dajin Gomo village of Sumaila eneo la Kano, Nigeria, Novemba 2, 2015.
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:28 0:00

Ukame, ardhi kugeuka jangwa, ukataji miti na mabadiliko ya hali ya hewa Kaskazini mwa Nigeria yamewalazimisha wafugaji kuhamia kusini wakitafuta maeneo ya malisho kwa mifugo.

Harakati hii imepelekea hasara ya zaidi ya maisha elfu 60 kwa mujibu wa spika wa Baraza la Wawakilishi la Nigeria.

Kuzungumzia suala hili, mradi wa kilimo na ufugaji ulizinduliwa huko Kano, na kuweka makazi, maeneo ya malisho na vituo vya ukusanyaji maziwa ili kuwazuia wafugaji kupambana na wakulima.

Ibrahim Garba Mohammed ni mratibu wa mradi wa kilimo na ufugaji katika jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Kano. Mradi unajumuisha maeneo ya malisho na makazi ya wafugaji wa Fulani ambayo yamefadhiliwa na “Lives, livelihood Funds” LLF na ‘Benki ya Maendeleo ya Kiislamu.’ Lengo ni kutokomeza ghasia kote Nigeria.

Mkuu wa Polisi Muhammad Musa Katsina (wapili kulia) akikabidhi ng'ombe waliokuwa wameibiwa kwa Zubairu Hamza, mwakilishi wa wilaya za Sumaila na Takai eneo la jimbo la Kano, Nigeria October 23, 2015. REUTERS/Stringer - RTX1SYRX
Mkuu wa Polisi Muhammad Musa Katsina (wapili kulia) akikabidhi ng'ombe waliokuwa wameibiwa kwa Zubairu Hamza, mwakilishi wa wilaya za Sumaila na Takai eneo la jimbo la Kano, Nigeria October 23, 2015. REUTERS/Stringer - RTX1SYRX

Ibrahim Garba Muhammad, Mratibu wa Mradi wa Kilimo na Ufufaji anaeleza: “Kuanzia sasa, tumewapatia chanjo zaidi ya mifugo milioni 3 katika jimbo hili. Kwa kuongezea, tumeweka maabara, ya kwanza ya aina yake kaskazini mwa Nigeria. Pia tumeandikisha wafanyakazi wa kijamii 220 kuangalia mifugo.”

Kwa miongo mingi, wakulima na wafugaji wamejihusisha na mzozo. Wakulima wanawashutumu wafugaji kwa kuiba mazao yao, wakati wafugaji walijihusisha na mashambulizi ya kulipiza kisasi wakiwalaumu wakulima kwa kunyakua maeneo ya malisho.

Kufanya mambo yawe mabaya zaidi, kuongezeka kwa hali ya ukavu, kaskazini mwa Nigeria, ukame na upanuzi wa ardhi ya kilimo kumepunguza ardhi ya malishi na kuchochea mizozo kwa kiasi fulani ya nchini Nigeria.

Mshauri wa kilimo Bello Abba Yakasai anasema kwamba kuhakikisha usalama kwa maeneo la malisho kwa ajili ya wafugaji ni muhimu sana kwa uendelevu wao, hasa katika kupambana na tishio la wizi wa ng’ombe.

Bello Abba Yakasai, Mshauri wa Kilimo anasema: “Serikali inatoa vipi usalama kwa makazi ya hawa Fulani? Wako katika mazingira hatarishi ya kulenga na wezi wamifugo. Unaweza kuwalinda vipi? Kama ukiniuliza nikae na nina ng’ombe kumi, nikae sehemu moja, na asubuhi ya pili, mtu anakuja na bunduki na kuchukua ng’ombe. Nina kinachofuata? Nitakufa.”

Mradi una azma ya kujibu baadhi ya maswali. Kwa miaka kadhaa, serikali ya Nigeria imekuwa ikitafuta suluhisho la kudum u kwa mzozo wa wakulima na wafugaji. Nigeria ina zaidi ya ng’ombe milioni 21 kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo ya Nigeria.

Kuwekwa kwa maeneo ya mifugo huko Kano kunawaruhusu wafugaji wa Fulani kama Muhammadu majo kubaki sehemu moja tu.

Muhammadu Majo, Mfugaji wa Fulani anafafanua: “Tunamshukuru Mungu kwamba tumekaa sehemu moja kwa amani, badala ya kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingi, ambapo ni hatari sana kwetu sisi hivi sasa. Sisi Wafulani tumeelezewa kama wahalifu, na watu wetu wameshambuliwa na hata kuuawa wakati wakipeleka mifugo kwenye maeneo mengine ya malisho.”

Sani Danladi Yadakwari anafanyakazi kwenye chama cha wakulima Nigeria.

Anaamini kwamba kuwapatia makazi wafugaji katika sehemu moja kumepunguza maafa na maisha ya watu.

Sani Danladi Yadakwari, Mkaguzi Mkuu, Chama cha Wakulima Nigeria anasema: "Kabla ya mradi wa kilimo na ufugaji, takriban watu 100 na malikadhaa ziliharibiwa kila mwaka kutokana na ukosefu wa barabara zinazopitika, uhusiano mbaya kati ya wafugaji na wakulima, na ukosefu wa maelewano miongoni mwa wafugaji kuhusu njia zilizovamiwa.”

Ujenzi wa shule, nyumba kwa ajili ya jamii za Fulani, pamoja na hospitali ya wanyama na vituo vya kukusanya maziwa, kumewapatia wafugaji vivutio vya ziada kubaki sehemu moja.

Hawataki tena kuzunguka kwenda sehemu za mbali kwa ajili ya malisho, kwa mujibu wa Umoja wa Wakulima, ghasia zimepungua huko Kano.

Ripoti ya mwandishi wa VOA Alhassan Bala

Forum

XS
SM
MD
LG