Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 00:13

Jeshi la Burkina Faso lazuia matangazo ya BBC na VOA kwa wiki mbili


FILE -Jeshi la Burkina Faso likijipanga katika mafunzo ya kijeshi ya kila mwaka yanayoendeshwa na Chuo cha Mafunzo cha Flintlock dhidi ya Ugaidi wa Kimataifa Internationl huko Jacqueville, Ivory Coast, on March 14, 2023.
FILE -Jeshi la Burkina Faso likijipanga katika mafunzo ya kijeshi ya kila mwaka yanayoendeshwa na Chuo cha Mafunzo cha Flintlock dhidi ya Ugaidi wa Kimataifa Internationl huko Jacqueville, Ivory Coast, on March 14, 2023.

Baraza Kuu la Mawasiliano la Burkina Faso (CSC) limetangaza kusimamisha matangazo na vipindi vya BBC/ Africa na VOA kufuatia habari iliyotangazwa kuhusu ripoti ya Human Rights Watch inayolishutumu Jeshi la Burkinabe kwa udhalilishaji mbalimbali wanaowafanyia raia.

Hatua ya CSC inahusisha amri ya kusimamisha mara moja kutangaza marejeo ya vipindi na kuamuru kusimamishwa kwa muda matangazo mengine ya vituo mbalimbali vya radio za kimataifa kwa wiki mbili. Pia tovuti na mitandao ya kidigitali ya BBC, VOA, na shirika la Human Rights Watch shughuli zao zimesimamishwa ndani ya Burkina Faso.

Katika matangazo ya habari hiyo iliyokuwa katika ripoti ya Human Rights Watch, VOA ilitafuta majibu kutoka kwa maafisa kadhaa wa Burkina Faso lakini hawakupata majibu yoyote.

VOA itaendelea na msimamo wake wa kuripoti kuhusu Burkina Faso na inakusudia kuendelea kutoa habari kamili na zisizoegemea upande wowote za shughuli mbalimbali zinazotokea nchini humo.

Forum

XS
SM
MD
LG