Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 28, 2024 Local time: 01:05

Raundi ya 16 Afcon: Nigeria na Cameroon kutoana jasho


Mshambuliaji wa Cameroon Vincent Aboubakar (kushoto) akiwa mazoezini kabla ya mechi ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2024 (CAN) kati ya Cameroon na Nigeria, mjini Bingerville, Januari 26, 2024.
Mshambuliaji wa Cameroon Vincent Aboubakar (kushoto) akiwa mazoezini kabla ya mechi ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2024 (CAN) kati ya Cameroon na Nigeria, mjini Bingerville, Januari 26, 2024.

Timu ya Nigeria itakutana na Cameroon Jumamosi  katika uwanja wa Felicia wa Abidjan, katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2024. Pambano linalosubiriwa kwa hamu.

Katika mkutano na wanahabari kabla ya mechi siku ya Ijumaa, Jose Peseiro, kocha wa Super Eagles, alisema Nigeria inalenga kushinda mchezo huo.

Kocha wa wa Cameroon Rigobert Song alisema ingawa anaiheshimu Nigeria, timu yake ilikuwa inajiadaa kuchukua ushindi.

Tulianza taratibu. Tunazidi kujijenga pole pole, na mechi ya Jumamosi itakuwa mchezo mwingine," Song alisema.

Timu zote mbili zimeanza kwa kusua sua kampeni yao. Nigeria ilimaliza ya pili katika Kundi A nyuma ya Equtorial Guinea, huku Cameroon ikinusurika chupuchupu kuondolewa kutokana na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Gambia.

Miamba hii miwili wa soka barani Afrika imekutana mara tatu kwenye hatua hiyo kubwa zaidi barani humo, huku Nigeria ikishinda 3-2 mwaka 2019 na 2-1 mwaka 2004 baada ya Cameroon kushinda 4-3 kupitia mikwaju ya penati kufuatia sare ya 2-2 miaka minne iliyopita.

Jumla ya michezo wamecheza 8 Nigeria ameshinda mara 4 na Cameroon ameshinda mara 2 na wametoka sare mara 2.

Forum

XS
SM
MD
LG