Rais wa Marekani Joe Biden, Jumatatu atakuwa na mazungumzo na Mfalme Abdullah wa pili wa Jordan, kwenye White House, mjini Washington DC, juu ya suala la kuachiliwa mateka waliopo Gaza, pamoja na kuongezeka kwa wasi wasi kutokana na operesheni za kijeshi za Israel kwenye mji wa bandari wa Rafah.