Jarida la weekendi linaangazia ushiriki wa vyama vya upinzani katika kupigania demokrasia Afrika Mashariki na jinsi ambavyo vitahakaikisha haviingiliwi na serikali katika shughuli zao.
Jarida la wikiendi linaangazia vita huko Sudan ambavyo vimepamba moto huku dunia ikionyesha kujitenga na mzozo huo. Tangu vita hiyo izuke mwaka mmoja uliopita takriban watu 16,000 wameuawa na wengine milioni 8.6 kupoteza makazi yao na kusababisha mgogoro mkubwa wa kibinaadamu
Jarida la Wikiendi linaangazia mgogoro wa kidiploamsia kati ya Somalia na Ethiopia kuhusiana na mikataba na ushirikiano kati ya Ethiopia na Somaliland pamoja na jimbo la Puntland.
Tume za uchaguzi za nchi Afrika Mashariki zimejikuta katika mzozo wa muda mrefu ya kuhakikisha zinasimamia uchaguzi na kuwa huru na wa haki.
Umoja wa Afrika umefanya marekebisho ya kanuni za uteuzi wa mwenyekiti wa tume ya umoja huo na kutoa fursa ya moja kwa moja kwa jumuiya ya Afrika Mashariki kushikilia nafasi hiyo. Kenya imemtangaza kiongozi wa upinzani Raila Odinga kugombea nafasi hiyo, na imeanza kampeni.
Jarida la Wikiendi linaangazia hali ya usalama nchini Haiti ambayo imeendelea kuzorota, na jitihada ya kurejesha utulivu wa kisiasa katika taifa hilo la Carribean.
Hii leo tunaangazia mgogoro wa bahari ya Shamu unavyoathiri njia hiyo ya majini kutokana na wanamgambo wa Houthi kurusha makombora na ndege zisizo na rubani zinazolenga meli za kibiashara, Tunajiuliza kwa kiwango gani wafanyabiashara ukanda wa Afrika Mashariki wameathirika?
Somalia imeingia mkataba wa ulinzi na Uturuki ikisisitiza kwamba inajiimarisha kijeshi kulinda mipaka yake baada ya Ethiopia kukubaliana na Somaliland kuunda jeshi la majini kwenye sehemu ya Somaliland, hatua ambayo Somalia inasema ni ya uchokozi.
Uchukuzi wa baharini unaendesha asilimia kubwa ya biashara duniani. Mataifa ya Afrika Mashariki yanatekeleza sera mbali mbali kuhakikisha wanafaidika na biashara kwa kuimarisha bandari zao na kuboresha uchumi kutokana na mapato ya bandari hizo.
Jarida la wikiendi linaangazia upanuzi na ujenzi wa haraka wa miji katika kanda ya Afrika Mashariki na athari zake kwa makazi, maendeleo ya miundombinu na mipango miji.
Wakati tatizo la ajira kwa vijana likiendelea kukua duniani kote, Jarida la Wikiendi linaangalia fursa zilizopo na namna gani vijana wanaweza kutatua tatizo hili kwa serikali zao.
Jarida la Wikiendi wiki hii linaangazia namna ambavyo vyombo vya usalama vinachukua hatua kuhakikisha kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki inakuwa salama.
Pandisha zaidi