Hii leo tunaangazia mgogoro wa bahari ya Shamu unavyoathiri njia hiyo ya majini kutokana na wanamgambo wa Houthi kurusha makombora na ndege zisizo na rubani zinazolenga meli za kibiashara, Tunajiuliza kwa kiwango gani wafanyabiashara ukanda wa Afrika Mashariki wameathirika?
Somalia imeingia mkataba wa ulinzi na Uturuki ikisisitiza kwamba inajiimarisha kijeshi kulinda mipaka yake baada ya Ethiopia kukubaliana na Somaliland kuunda jeshi la majini kwenye sehemu ya Somaliland, hatua ambayo Somalia inasema ni ya uchokozi.
Uchukuzi wa baharini unaendesha asilimia kubwa ya biashara duniani. Mataifa ya Afrika Mashariki yanatekeleza sera mbali mbali kuhakikisha wanafaidika na biashara kwa kuimarisha bandari zao na kuboresha uchumi kutokana na mapato ya bandari hizo.
Jarida la wikiendi linaangazia upanuzi na ujenzi wa haraka wa miji katika kanda ya Afrika Mashariki na athari zake kwa makazi, maendeleo ya miundombinu na mipango miji.
Wakati tatizo la ajira kwa vijana likiendelea kukua duniani kote, Jarida la Wikiendi linaangalia fursa zilizopo na namna gani vijana wanaweza kutatua tatizo hili kwa serikali zao.
Jarida la Wikiendi wiki hii linaangazia namna ambavyo vyombo vya usalama vinachukua hatua kuhakikisha kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki inakuwa salama.
Wiki tunaangazia nafasi ya wanawake katika siasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na changamoto wanazopitia mara baada ya kumalizika uchaguzi mkuu. Mjadala huu unajikita katika nafasi ya wanawake na tofauti za kijinsia kama inavyoshuhudiwa katika upatikanaji uongozi wa kisiasa.
Mivutano imezidi kushika kasi katika jumuiya ya Afrika Mashariki na hii inaanza kuzua wasiwasi kwamba huenda historia ya utangamano wa jumuiya hiyo ukaingia shubiri.
Mpango mpya wa kutohitajika kwa visa kusafiri nchini Kenya sasa unawataka wageni kutoka nje ya Kenya kutuma ombi la hitaji ya pasi ya kielektroniki (ETA) siku tatu kabla ya kufunga safari kuzuru Kenya.
Wakati uchumi na maisha ya raia wa Afrika Mashariki ukiwa unategemea zaidi sekta ya kilimo, ambayo inajumuisha asilimia 25 hadi 40 ya mapato ya EAC ikitokana na uzalishaji Chakula.
Kipindi cha Jarida la Wikiendi linaangazia uchaguzi mkuu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku hali ya utulivu wa wananchi wa nchi hiyo ukiwa au ukiendelea kuwa rehani.
Jarida la Wikiendi linaangazia ubinafsishaji wa mashirika ya umma, kitendo cha kuyafanya mashirika hayo yaliyokuwa yanaendeshwa na serikali kuwa kwenye mikono ya watu binafsi kwa ajili ya kuongeza ufanisi na kuvutia uwekezaji zaidi.
Pandisha zaidi