Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 00:53

China yawawekea vikwazo wanasisa wa Taiwan


FILE PHOTO: Wellington Koo, mmoja wa maafisa wa wa seikali ya Taipei.
FILE PHOTO: Wellington Koo, mmoja wa maafisa wa wa seikali ya Taipei.

China imewawekea vikwazo kadhaa wanasiasa wa Taiwan, vikiwa ni pamoja na vya viza za kusafiria, huku ikiongeza shinikizo kwa kisiwa hicho, kinachojitawala, na kama majibu kwa mfululizo wa ziara zilizofanywa kwenye kisiwa hich, na wabunge wa Marekani.

Vikwazo hivyo vinakuja siku moja baada ya China kufanya mazoezi zaidi ya kijeshi katika bahari na anga zinazoizunguka Taiwan, kujibu kile ilichokiita "kula njama na uchochezi kati ya Marekani na Taiwan."

Hakukuwa na taarifa kuhusu muda na ukubwa wa mazoezi hayo ya China. Vikwazo hivyo vimetangazwa katika siku ambayo wajumbe wa bunge la Marekani, walikutana na Rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen, na baada ya ziara kama hiyo, ya Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi, mjumbe wa ngazi ya juu zaidi wa serikali ya Marekani kutembelea Taiwan katika kipindi cha miaka 25.

Serikali ya China inapinga Taiwan kuwa na mawasiliano yoyote rasmi, na serikali za kigeni kwa sababu inachukulia Taiwan kuwa himaya yake, na taarifa zake za hivi karibuni zimekuwa zikisisitiza tishio lake la kuchukua kisiwa hicho kwa nguvu za kijeshi.

Ziara ya Pelosi ilifuatiwa na karibu wiki mbili za mazoezi ya kutishia ya kijeshi ya China ambayo ni pamoja na kurusha makombora kwenye kisiwa hicho na uvamizi wa meli za jeshi la wanamaji na ndege za kivita katikati mwa Mlango wa bahari wa Taiwan ambao kwa muda mrefu umekuwa kizuizi kati ya pande zote.

XS
SM
MD
LG