Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 29, 2024 Local time: 07:31

Kenya yaahidi kufanya kazi na mataifa ya EAC ili kuimarisha uhusiano

Rais William Ruto wa Kenya
Rais William Ruto wa Kenya

Waziri Mkuu wa Kenya Musalia Mudavadi ambaye pia ndiye Waziri wa masuala ya kigeni amethibitisha Kenya kujitolea kufanya kazi na mataifa yote wanachama katika kuimarisha ushirikiano na ustawi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Mudavadi ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje na Diaspora, amesema kuwa nchi zote wanachama zinapaswa kukutana na kutafakari mwelekeo wa EAC, inayohusu ustawi, ushindani, usalama, utulivu na umoja wa kisiasa wa Afrika Mashariki ili umoja wa kikanda uwe dhabiti.

Mudavadi alizungumza hayo alipokutana na mwenzake wa Tanzania Dkt January Makamba kando ya mkutano wa Mawaziri wa Mkutano wa Nchi Wanachama wa Nchi Zisizofungamana na Siasa (NAM) unaofanyika Kampala, Uganda.

Mawaziri hao wawili wa Mambo ya Nje walikubaliana kuendeleza mazungumzo ya kina baina ya nchi hizo mbili kama hatua ya kuimarisha na kuendeleza sera za kidiplomasia za kigeni za Kenya na Tanzania.

Forum

XS
SM
MD
LG