Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 07, 2024 Local time: 09:25

ADF yashutumiwa kuhusika na mauaji Uganda


Kamanda wa ADF Kyoto Abdul Rashid anayejulikana kwa jina la "Njovu"akiwa mahakamani huko Kampala Novemba 31 2023. Picha na REUTERS/Abubaker Lubowa
Kamanda wa ADF Kyoto Abdul Rashid anayejulikana kwa jina la "Njovu"akiwa mahakamani huko Kampala Novemba 31 2023. Picha na REUTERS/Abubaker Lubowa

Takriban watu watano wameuawa, akiwemo diwani, baada ya washukiwa waasi kutoka kundi la Allied Democratic Forces (ADF) lenye uhusiano na Islamic State kushambulia eneo la Magharibi mwa Uganda Jumatatu jioni, mbunge wa eneo hilo ameliambia Shirika la habari la Reuters.

Allied Democratic Forces (ADF), iliundwa kama kundi la uasi dhidi ya Kampala katika miaka ya katikati ya 1990, na awali lilipambana na serikali ya Rais Yoweri Meseveni kutoka katika kambi zilizoko katika milima ya Rwenzori.

Siku ya Jumatatu majira ya saa nne usiku, kundi hilo la waasi liliivamia parokia ya Kyabandara katika wilaya ya Kamwenge Mgaharibi mwa Uganda, alisema mbunge Cuthbert Abigaba.

Washambuliaji hao walimuua diwani wa eneo hilo ambaye alikutwa kwenye mgahawa mdogo kando ya barabara alikokuwa akifanyakazi, akiwa na wateja wake wanne ambao walikuwa wameketi kwa ajili ya kupata chakula, alisema.

“Baada ya mauaji, waliuchoma moto mgahawa na pia kupora vitu katika maduka yaliyoko jirani kabla ya kukimbia” alisema Abigaba.

Naibu msemaji wa jeshi la Uganda Deo Akiiki, alithibitisha shambulio hilo na kusema watatoa taarifa zaidi baadaye.

Baada ya kuundwa kwake, ADF hatimaye lilisambaratishwa na jeshi na waliobaki walikimbialia Mashariki mwa Congo ambako walianzisha mashambulizi mabaya katika maeneo yote yaliyoko huko Congo na Uganda.

Uganda ilianzisha kampeni ya anga na ardhini dhidi ya ADF nchini Congo Mwaka 2021.

Meseveni alisema operesheni hiyo ilifanikiwa kuuwa kundi kubwa la waasi wakiwemo baadhi ya makamanda.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG