Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 27, 2024 Local time: 22:25

China inasema itaondoa ushuru uliowekwa kwa mvinyo wa Australia


Mfano wa mvinyo wa Australia ambao China inasema inaondoa ushuru wa bidhaa hizi
Mfano wa mvinyo wa Australia ambao China inasema inaondoa ushuru wa bidhaa hizi

China iliweka ushuru kwa mvinyo wa Australia mwaka 2020 wakati wa mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili

China imesema itaondoa ushuru uliowekwa kwa mvinyo wa Australia zaidi ya miaka mitatu iliyopita, ikiwa ni ishara ya kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Wizara ya Biashara ya China imesema uamuzi huo utaanza kutekelezwa siku ya Ijumaa.

China iliweka ushuru kwa mvinyo wa Australia mwaka 2020 wakati wa mzozo wa kidiplomasia juu ya msaada wa Australia kwa uchunguzi wa kimataifa kuhusu asili ya COVID-19. Ushuru wa mvinyo wa Australia uliongezeka zaidi ya asilimia 200. Wazalishaji wa mvinyo wa Australia walipigwa vibaya sana kutokana na ushuru huo, ambapo China ilikuwa kituo cha juu cha usafirishaji mvinyo nchini Australia.

Serikali ya Australia imekaribisha uamuzi huo ikisema katika taarifa kwamba ushuru huo uliondolewa katika wakati muhimu kwa sekta ya mvinyo ya Australia. He Yadong, msemaji wa Wizara ya Biashara ya China, alisema China na Australia ni washirika muhimu wa kibiashara wa kila mmoja.

Tuko tayari kufanya kazi na Australia kutatua wasiwasi wa kila mmoja kupitia mazungumzo na mashauriano, na kwa pamoja kukuza maendeleo thabiti na yenye afya katika mahusiano ya kiuchumi na biashara ya nchi mbili, alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG