Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 27, 2024 Local time: 19:15

Hali ya utulivu yaripotiwa mjini Khartoum


Moshi ukifuka wakati mapigano yakiendelea huko Khartoum terehe 9 Juni, 2023. Picha na AFP.
Moshi ukifuka wakati mapigano yakiendelea huko Khartoum terehe 9 Juni, 2023. Picha na AFP.

Wakazi wameripoti hali ya utulivu katika mji mkuu wa Sudan Khartoum Jumamosi tangu kuanza kutekelezwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa saa 24 kati majenerali wawili wanaopigana, lakini watu wachache wanaamini kuwa sitisho la mapigano litadumu.

Mapigano yamepamba moto katika taifa hilo la Afrika Kaskazini tangu katikati mwa mwezi Aprili, wakati mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani Mohamed Hamdan Dagalo, ambaye anaongoza kikosi cha dharura cha (RSF), waliposhambuliana.

Makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano yalifikiwa na kukiukwa tangu mzozo ulipozuka, na Marekani iliwawekea vikwazo majenerali hao hasimu baada ya juhudi za mwisho za kusitisha mapigano kukwama mwishoni mwa mwezi Mei.

Mashambulizi ya anga na mizinga ambayo yamekuwa yakiutikisha mji wa Khartoum kila siku yamepungua angalau kwa muda, na kuruhusu raia waliokwama katika mapigano kutoka nje na kununua bidhaa zinazohitajika sana.

Katika soko moja la Khartoum, watu walionekana wakihangaika kutafuta matunda na bidhaa nyingine msingi.

Forum

XS
SM
MD
LG