Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 27, 2024 Local time: 12:49

Hezbollah yafanya mashambulizi kaskazini mwa Israel


Moshi ukipaa angani kufuatia shambulizi la Israel kusini mwa Lebanon, Machi 10, 2024. Picha ya maktaba.
Moshi ukipaa angani kufuatia shambulizi la Israel kusini mwa Lebanon, Machi 10, 2024. Picha ya maktaba.

Wanamgambo wa Hezbollah wa Lebanon, Jumatano wamefanya mashambulizi ya roketi kaskazini mwa Isreal, wakijibu mashambulizi ya anga ya  Israel yaliyouwa watu 7 kusini mwa Lebanon.

Jeshi la Israel limesema kwamba mashambulizi yake yalilenga jengo la kijeshi ambapo mwanachama wa kundi la wanamgambo la Jamaa al-Islamiya, aliuwawa, akishutumiwa kuongoza mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Israel. Shirika la habari la AFP limemnukuu afisa mmoja wa Jamaa al-Islamiya akisema kuwa watu 7 waliuwawa kwenye kijiji cha Hebbariyeh, vyanzo vya usalama vya Lebanon vikitoa idadi sawa na hiyo kwa shirika la habari la Reuters.

Mashambulizi hayo ya mpakani ndiyo hatua ya karibuni zaidi wakati Israel ikiendeleza kampeni yake inayolenga kuliangamiza kundi la kigaidi la Hamas, ambalo ni mshirika wa Hezbollah huko Ukanda wa Gaza. Jeshi la Israel Jumatano pia limeripoti kufanya operesheni za ardhini karibu na hospitali ya Shifa, kaskazini mwa Gaza, wakati pia likifanya mashambulizi ya anga na ardhini kwenye eneo la Khan Younis, lililopo kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Juhudi za kupata sitisho la muda la mapigano na mapendekezo ambayo yanajumuisha kuachiliwa kwa matekan walioko huko Gaza, pamoja na kuongezza misaada wa kibinadamu kwa raia wa Palestina yanaonekana kukaribia kufikiwa hata baada ya azimio la Baraza la Usalama la UN kutaka sitisho la haraka la mapigano hayo.

Forum

XS
SM
MD
LG