Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 28, 2024 Local time: 10:36

Israel imeripoti mapigano katika eneo la hospitali ya Shifa huko Gaza City


Moshi umetanda wakati wa shambulizi la Israel katika hospitali ya Shifa huko Gaza City. March 28, 2024. (Photo by AFP)
Moshi umetanda wakati wa shambulizi la Israel katika hospitali ya Shifa huko Gaza City. March 28, 2024. (Photo by AFP)

Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imesema watu zaidi ya 32,000 wameuawa wakati wa mashambulizi ya Israel

Jeshi la Israel limeripoti leo Alhamisi mapigano katika eneo la hospitali ya Shifa huko Gaza City, pamoja na Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Wizara ya afya katika Ukanda wa Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema kuwa Wa-palestina 62 wameuawa katika siku moja iliyopita. Wizara hiyo imesema watu zaidi ya 32,000 wameuawa wakati wa mashambulizi ya Israel ambayo yalianza mwezi Oktoba baada ya shambulio la Hamas dhidi ya Israel ambalo liliuwa watu 1,200.

Katika hatua nyingine, Israel imekubali Jumatano kutuma wapanga mikakati wake wa kivita mjini Washington kujadili nia yake ya kuanzisha mashambulizi ya ardhini dhidi ya wanamgambo wa Hamas katika mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah.

Forum

XS
SM
MD
LG