Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 29, 2024 Local time: 04:45

Kenya yatoa miili ya kwanza ya mauaji ya kidini kwa familia


Wanafamilia moja wakiomboleza baada ya kupokea mabaki ya wanafamilia kadhaa ambao walikuwa waathiriwa wa ibada ya kukaa na njaa nchini Kenya.
Wanafamilia moja wakiomboleza baada ya kupokea mabaki ya wanafamilia kadhaa ambao walikuwa waathiriwa wa ibada ya kukaa na njaa nchini Kenya.

Maafisa wa usalama wa Kenya  Jumanne walianza kutoa miili ya waathiriwa kadhaa wa mauwaji yaliyofanywa na dhehebu lililowataka waumini wao wajiuwe kwa kukaa na njaa ili kwenda kukutana na Yesu

Maafisa wa usalama wa Kenya Jumanne walianza kutoa miili ya waathiriwa kadhaa wa mauwaji yaliyofanywa na dhehebu lililowataka waumini wao wajiuwe kwa kukaa na njaa ili kwenda kukutana na Yesu.

Kutolewa kwa miili hiyo inafanyika karibu mwaka mmoja baada ya kugunduliwa kwa makaburi ya halaiki katika kesi mbaya ambayo ilishangaza ulimwengu.

Familia moja ilipokea miili minne iliyokuwa imepakiwa kwenye gari la kubebea maiti kutoka kwa chumba cha kuhifadhia maiti katika mji wa Malindi, huku wapendwa wao wakiomboleza.

Hiyo ni miili ya kwanza kukabidhiwa familia baada ya miezi kadhaa ya kazi ngumu ya kutambua wathiriwa kupitia utafiti wa vinasaba DNA.

Forum

XS
SM
MD
LG