Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 28, 2024 Local time: 04:19

Kocha wa timu ya taifa ya Ghana afutwa kazi baada ya Black Stars kuondoka mapema katika michuano ya AFCON


Meneja wa timu ya taifa ya Ghana Chris Hughton wakati wa mechi kati ya Ghana na Cape Verde mjini Abidjan, Januari 14, 2024.
Meneja wa timu ya taifa ya Ghana Chris Hughton wakati wa mechi kati ya Ghana na Cape Verde mjini Abidjan, Januari 14, 2024.

Chama cha soka nchini Ghana kimemfuta kazi kocha wa timu ya taifa Chris Hughton baada ya timu hiyo kuaga mashindano ya kombe la mataifa barani Afrika katika mzunguko wa makundi.

The Black Stars walifungwa na Cape Verde mabao 2 kwa 1 katika mechi ya ufunguzi nchini Ivory Coast na kwenda sare na Misri na Msumbiji, na waliondolewa katika kundi B jana Jumanne kufuatia matokeo ya michezo mingine.

Hughton, beki wa zamani wa Tottenham na kocha wa Brighton na New Castle, aliteuliwa kuwa kocha wa Ghana mwezi Februari mwaka wa 2023.

“Chama cha soka cha Ghana kinataka kutangaza kwamba Chris Hughton ameachishwa kazi kama meneja mkuu wa timu ya taifa kuanzia hivi sasa,” chama hicho kimesema katika taarifa Jumanne.

Forum

XS
SM
MD
LG