Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 28, 2024 Local time: 04:48

Mahakama ya Iran yamuhukumu kifo mkuu wa polisi kwa kumuua mwandamanaji


Maandamano ya Iran mwaka 2022
Maandamano ya Iran mwaka 2022

Mahakama ya Iran ilimuhukumu kifo mkuu wa polisi kaskazini mwa Iran baada ya kushtakiwa kwa kumua mtu wakati wa maandamano makubwa mwaka 2022, vyombo vya habari vya ndani viliripoti Jumatano.

Mkuu wa polisi Jafar Javanmardi alikamatwa mwezi Disemba mwaka 2022 juu ya mauaji ya mwandamanaji wakati wa maandamano makubwa yaliyochochewa na kifo cha Mahsa Amini akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Amini, Muiran Mkurdi mwenye umri wa miaka 22, alifariki mwezi Septemba 2022 akiwa chini ya ulinzi wa polisi kufuatia kukamatwa kwake kwa madai ya kukiuka sheria kali ya nchi kuhusu mavazi kwa wanawake.

Javanmardi amehukumiwa kifo “ kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu ya kulipiza kisasi, inayojulikana kama ‘qisas sharia’, kwa shtaka la mauaji ya kukusudia,” wakili wa familia ya mwathirika, Majid Ahmadi, aliliambia gazeti linalotetea mageuzi la Shargh.

Mwandamanaji, Mehran Samak, mwenye umri wa miaka 27, alifariki kutokana na majereha aliyoyapata baada ya kupigwa risasi wakati wa maandamano katika mji wa kaskazini wa Bandar Anzali tarehe 30 Novemba, mwaka 2022.

Forum

XS
SM
MD
LG