Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 29, 2024 Local time: 04:44

Mlipuko wa gesi waua na kujeruhi watu 280 Nairobi


Watu wakikimbilia kuokoa maisha yao kufuatia mfululizo wa milipuko iliyosababisha moto katika eneo la Embakasi Nairobi Februari 2, 2024. Picha na LUIS TATO / AFP.
Watu wakikimbilia kuokoa maisha yao kufuatia mfululizo wa milipuko iliyosababisha moto katika eneo la Embakasi Nairobi Februari 2, 2024. Picha na LUIS TATO / AFP.

Gari lilokuwa lililojaa mitungi ya gesi limelipuka katika makazi yenye msongamano wa watu, kuwaka moto na kuteketeza nyumba na ghala katika mji kuu wa Nairobi nchini Kenya mapema Ijumaa. Mliuko huo umejeruhi watu 280 na kusababisha vifo vya watu wasiopungua watatu, serikali imesema siku ya Ijumaa

Msemaji wa serikali, Isaac Mwaura amesema huenda idadi kubwa ya wakazi walikuwa ndani ya nyumba zao wakati moto uliposhika kwenye nyumba zao wakati wa usiku. Eneo la makazi lililokumbwa na mkasa liko upande wa kusini mashariki mwa Nairobi, ambako mali nyingi na magari ziliathiriwa na moto na kusababisha wakati kukimbia kuokoa maisha yao.

Wafanyakazi wa zimatoto waliweza kuudhibiti moto huo majira ya saa tatu asubuhi , zaidi ya saa tisa baada ya moto huo kuzuka katika eneo la Mradi huko Embakasi, kulingana na mwandishi wa habari wa AFP aliyekuwepo katika eneo la tukio.

Mwanamke akiangalia nyumba na maduka yaliyoteketea.
Mwanamke akiangalia nyumba na maduka yaliyoteketea.

Lori lililosababisha mlipuko huo, lilikuwa na namba za usajili zisizojulikana na lilikuwa limejaa gesi iliyosababisha moto mkubwa na mtungi wa gasi uliruka na kuanzisha moto ambao uliteketeza ghala ya vitambaa na nguo la Oriental Godown, alisema Mwaura.

Magari mengine kadhaa na biashara yameharibiwa na moto huo ambao ulianza majira ya saa tano na nusu usiku, siku ya Alhamisi katika eneo la Mradi katika kitongoji cha Embakasi mjini Nairobi.

Katika eneo la tukio, baada ya kupambazuka, nyumba na maduka kadhaa yalikuwa yameteketea. Gari linaloaminika kuanzisha mlipuko huo lilirushwa pembeni na mabaki yake yalikuwa barabarani.

Watu wakiangalia uharibifu iliosababishwa na moto huo mkubwa
Watu wakiangalia uharibifu iliosababishwa na moto huo mkubwa

Paa la jengo la ghorofa nne la makazi ya watu lililokuwa kiasi cha mita 200 kutoka eneo la tukio la mlipuko, lilivunjwa na mtungi wa gasi. Nyaya za umeme ziliangushwa chini. Hakuna kilichosalia kwenye ghala iliyoteketezwa na moto isipokuwa mabaki ya magari kadhaa makubwa.

Alfred Juma, mwanasiasa anayenyanyukia, amesema alisikia mlio mkubwa kutoka kwenye mtungi wa gesi katika ghala karibu na nyumba yake. “nilianza kuwaamsha majirani na kuwataka waondoke,” alisema Juma.

Alisema aliwachukua watoto wawili na kujificha chini ya shimo la maji taka mpaka milipuko hiyo ilipokwisha. Familia yake haikuwepo katika eneo hilo, lakini Juma amepoteza kila kitu katika moto huo isipokuwa nguo alizokuwa amevaa.

Baadhi ya taarifa za habari hii zinatoka shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG