Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 30, 2024 Local time: 03:30

MWAKA MMOJA WA VITA SUDAN


Kamanda wa jeshi la Sudan Abdel-Fattah Burhan, Khartoum, akiwa Sudan, Dec. 5, 2022.
Kamanda wa jeshi la Sudan Abdel-Fattah Burhan, Khartoum, akiwa Sudan, Dec. 5, 2022.

Haya ni maelezo kwa ufupi kuhusu jeshi la Sudan na kikosi cha kijeshi cha Rapid support forces - RSF ambao wamekuwa wakipigana kwa muda wa mwaka mmoja sasa na kupelekea mateso makubwa kwa nchi yao.

Mapigano hayo pia yamepelekea kuzuka tena mapigano mabaya katika eneo la Dafur. Mamilioni ya watu wamekoseshwa makao.

Makamanda wa jeshi la taifa na wa kikosi cha RSF walikuwa washirika wakubwa chini ya utawala wa rais wa zamani Omar Al-Bashir na walishirikiana kumuondoa madarakani mwaka 2019.

Walishirikiana pia kupindua utawala wa kiraia mwaka 2021.

JESHI LA KITAIFA

Jeshi la Sudan linaongozwa na Generali Abdel Fattah al-Burhan. Ana idadi kubwa ya wanajeshi ikilinganishwa na kikosi cha RSF. Ana silaha na ndege za kivita.

Burhan amekuwa karibu na utawala wa Sudan kwa miongo kadhaa. Alizaliwa mwaka 1960 kaskazini mwa Khartoum, karibu na nyumbani kwa Bashir na kazi yake yote imekuwa katika jeshi.

Jeshi la Sudan limekuwa likishirikiana na vikundi vya wapiganaji ikiwemo kikosi cha RSF katika eneo la Dafur, mara nyingi kwa maslahi ya kiuchumi.

Chini ya utawala wa Bashir, Burhan alikuwa kamanda katika eneo la Dafur ambapo serikali ilikuwa na lengo kubwa la kuzima harakati za mapinduzi, katika mapigano yaliyopelekea karibu watu milioni 2 kukoseshwa makao na 300,000 kufariki kufikia mwaka 2008.

Burhan pia alianzisha ushirikiano na nchi za Ghuba ambapo alikuwa anatuma wanajeshi katika muungano wa kijeshi ulioongozwa na Saudi Arabia kupigana nchini Yemen.

Burhan alisema kwamba alikuwa miongoni mwa maafisa wa kijeshi waliomwambia Bashir kwamba aondoke madarakani. Baadaye, Burhan alionekana kama kiongozi wa Sudan baada ya Bashir.

Katika siku za mwanzoni za vita, jeshi la taifa lilizidiwa na kikosi cha RSF katika mji mkuu wa Khartoum, na baadaye katika Dafur na el-Gezira kusini mwa Khartoum.

Mapema kwama huu, jeshi la Sudan lilidhibithi Omdurman kutoka kwa RSF.

Ripoti ya shirika la habari la Reuters inasema kwamba jeshi linatumia ndege zisizo na rubani zilizotengenezwa Iran.

Jeshi pia limepokea usaidizi kutoka kwa mataifa ya nje yakiwemo Misri na sasa linadhibithi sehemu kubwa za kaskazini na mashariki ikiwemo bandari ya Sudan na sehemu za bahari ya shamu.

Raia wa Sudan wameshutumu jeshi kwa kuua raia na kurusha makombora kiholela katika mji mkuu wa Khartoum na sehemu zingine kulipo na wapiganaji wa RSF. Jeshi limefutilia mbali madai hayo.

KIKOSI CHA RSF

Kikosi cha wapiganaji wa Rapid response forces - RSF, kinaongozwa na tajiri ambaye alikuwa kiongozi wa kikundi cha wapiganaji, Generali Mohamed Hamdan Dagalo, maarufu kama Hemedti.

Wachambuzi wanakadiria kwamba kikosi hicho kina wapiganaji karibu 100,000 (kabla ya vita kuanza) na kambi katika sehemu tofauti za Sudan.

Hemedti hakumaliza masomo. Umri wake unaaminika kuwa katika miaka ya 40. Alikuwa muuzaji wa ngamia mjini Dafur.

Inaripotiwa kwamba alianza mapigano baada ya msafara wa magari yake yaliyokuwa yamebeba ngamia kuelekea sokoni ulipovamiwa. Mapigano yaliua watu 60 kutoka kwa familia yake na alipoteza mifugo.

Ujuzi wake wa mapigano uliongezeka, alipojiunga na serikali kuvunja maandamano na mapigano ya Dafur mwaka 2003.

Makundi ya wapiganaji baadaye yalipewa jina la Janjaweed kutokana na namna walivyokuwa wakipigana bila uoga.

Mahakama ya uhalifu ya kimataifa ICC, ilishutumu maafisa wa serikali na viongozi wa Janjaweed, bila kumtaja Hemedti, kwa mauaji ya halaiki ya watu na uhalifu mwingine wa kivita.

Kundi la RSF limeimarika na kutambuliwa mnamo mwaka 2017 kuwa kikosi cha kijeshi, kilichoungwa mkono na Bashir.

Hemedti amekuwa mfanyabiashara maarufu katika uchimbaji dhahabu, ujenzi wa miundo mbinu, biashara ya mifugo miongoni mwa nyingine.

Raia wa Sudan, makundi ya kutetea haki za kibiandamu na wataalam wa umoja wa mataifa wameshutumu kikosi cha RSF na makundi mengine ya wapiganaji yanayoshirikiana na kikosi hicho kwa kulenga makabila katika vita ndani ya Dafur. RSF kimepuuzilia mbali madai hayo.

Kuna taarifa kwamba washirika wakubwa wa Hemedti ni Umoja wa falme za kiarabu. UAE imepuuzilia mbali ripoti za kutoa silaha kwa RSF.

Forum

XS
SM
MD
LG