Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 28, 2024 Local time: 16:19

RSF yalaumiwa kukata mawasiliano Sudan


Kiongozi wa Kikosi cha Dharura cha Sudan, Mohammed Hamdan Dagalo
Kiongozi wa Kikosi cha Dharura cha Sudan, Mohammed Hamdan Dagalo

Kikosi cha Dharura cha Sudan RSF kinatuhumiwa hivi sasa kusitisha huduma za mawasiliano na hivyo kuharibu usambazaji wa misaada na kuzusha hofu miongoni mwa wakazi takribani milioni 50 kuwasialiana na jamaa zao walioko nje ya nchi.

RSF imekuwa ikipambana na jeshi la Sudan kutaka kuitawala nchi hiyo tangu April mwaka 2023, katika vita ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya raia, mamilioni kupoteza kazi na kuzusha janga la njaa.

Vyanzo vinne vya makampuni ya mawasiliano vimeliambia shirika la habari la Reuters kuwa RSF ilianza kuzima mitandao Februari 5, na kumalizia kabisa siku mbili baadaye.

Baada ya miezi kumi ya mgogoro, kikosi cha RSF kinadhibiti sehemu kubwa ya mji mkuu wa Khartoum na baadhi ya miondo mbinu ya mji huo, yakiwemo makao makuu ya makampuni ya mawasiliano.

RSF haikutoa majibu kuhusiana na tuhuma hizo, chanzo cha RSF kimesema Februari 5 kuwa wanamgambo hao hawahusiki na kukatika kwa mawasiliano hayo.

Makampuni ya mawasialiano yanailaumu hali iliyopo kuwa inatokana na ukosefu wa mafuta na mazingira magumu ya kazi.

Forum

XS
SM
MD
LG