Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 28, 2024 Local time: 23:40

Haiti imeomba msaada, nani yupo tayari na nani atatoa ufadhili?


Waendesha piki piki wakipita karibu na moto uliowashwa na waandamanaji mjini Port-au-prince, Haiti, March 7, 2024 PICHA: Reuters
Waendesha piki piki wakipita karibu na moto uliowashwa na waandamanaji mjini Port-au-prince, Haiti, March 7, 2024 PICHA: Reuters

Serikali ya Haiti iliomba rasmi msaada wa usalama kutoka kwa nchi zote kote duniani, zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Wakati huo, serikali ya Haiti ilitaka msaada wa polisi au kijeshi kukabiliana na magenge ya uhalifu katika mji mkuu wa Port-au-prince.

Kufikia sasa, ahadi ni nyingi kuliko matendo.

Waziri mkuu wa Hiti Ariel Henry amekuwa nchini Kenya wiki iliyopita ambapo alisaini makubaliano ya kiusalama na uongozi wa Kenya.

Wakati Ariel alikuwa Kenya, mapigano na ghasia viliongezeka kwa kasi sana nchini mwaka. Watu waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito walivamia magereza yenye idadi kubwa ya wafungwa na kuwaachilia huru.

Maafisa wa Haiti wametangaza dharura ya kitaifa huku maelfu ya watu waliokoseshwa makao wakiishi katika kambi za muda katika mji mkuu.

Umoja wa mataifa umesema kwamba maelfu ya watu wamekoseshwa makao na maelfu wameuawa katika ghasia nchini Haiti. Kuna ripoti za unajisi, dhuluma na watu kutekwa nyara katika kila sehemu ya nchi.

Hali tete, wimbi la wakimbizi, ukosefu wa imani

Rais wa Haiti Ariel Henry, aliomba msaada wa kiusalama kwa mara ya kwanza mnamo Oktoba 2022 ili kusaidia polisi wa Haiti kukabiliana na magenge ya uhalifu ambayo yalikuwa yanaimarika kwa kasi sana nchini humo hasa katika mji mkuu wa Port-au-Prince na kupelekea hali mbaya ya kibinadamu.

Mwaka mmoja baadaye, Umoja wa mataifa ulipitisha azimio la kuidhinishwa kikosi maalum cha usalama kwa ajili ya Haiti.

Hatua ya umoja wa mataifa ilitoa fursa ya kuanza kwa mchakato wa kutumwa kikosi maalum cha usalama Haiti, ufadhili wa kikosi hicho na kuanza kupokea orodha ya nchi ambazo zipo tayari kusaidia Haiti.

Nchi zimesita kujitolea. Baadhi zimeeleza kutokuwa na Imani na serikali ya Waziri mkuu Ariel Henry huku nchi hiyo ikishuhudia maandamano.

Idadi kubwa ya raia wa Hiati, walio ndani na nje ya nchi, wana wasiwasi na mpango wa kutuma walinda usalama nchini Haiti, ikitiliwa maanani kwamba hii sio mara ya kwanza Umoja wa mataifa umewahi kuidhinisha hatua ya kutuma kikosi cha usalama nchini humo.

Kikosi cha awali kuwahi kutumwa Haiti, badala yake kilikumbwa na kashfa za ngono huku nchi ikikabiliwa na mlipuko mkubwa wa kipindupindu.

Kenya, ilikubali kutuma polisi wake. Ahadi ya Kenya ilitolewa mwaka uliopita.

Hata hivyo, ahadi ya serikali ya Kenya ilizuiliwa na amri ya mahakama iliyotaka serikali ya Haiti kufanya kwanza makubaliano ya moja kwa moja na Kenya.

Henry alikuwa Kenya wiki iliyopita ambapo alisaini makubaliano hayo huku mapigano makali yakiendelea nchini mwake.

Henry aliwasili Puerto Rico mnamo Jumanne, baada ya vyombo vya habari kutipoti kwamba jamhuri hiyo ya Dominica, ilimzuia kuingia Hiati kwa kutumia anga yake.

Nchi gani zipo tayari kutuma walinda usalama Haiti?

Mwezi uliopita, Umoja wa mataifa ulisema kwamba nchi tano tayari zimeasilisha ahadi rasmi ya kutuma vikosi vya usalama.

Benin ndiyo inaongoza kwa idadi ya walinda usalama. Inatuma maafisa 1,500.

Chad, Bangladesh na Barbados zimeahidi kutuma walinda usalama lakini hakuna taarifa kamili kuhusu idadi yao ya walinda usalama wanaotumwa Haiti.

Bahamas iliahidi kutuma walinda usalama 150.

Kenya imeahidi kuongoza kikosi hicho kwa idadi ya polisi 1000.

Mapema mwaka uliopita, wanasiasa katika bunge la Kenya waliripoti kwamba Burundi na Senegal zilikuwa zimeahidi kutuma maafisa wake.

Vyombo vya habari vya Belize vimeripoti kwamba nchi hiyo imeahidi kutuma wanakeshi 50.

Waziri mkuu wa Antigua na Barbuda ameahizi kutuma wanajeshi. Hajasema idadi.

Vyombo vya habari vya Suriname pia vimeripoti kwamba nchi hiyo ipo tayari kutuma walinda usalama.

Kulingana na kanuni za umoja wa mataifa, nchi zinahitajika kumwarifu rasmi katibu mkuu iwapo zitatuma walinda usalama nchini Haiti.

Hakuna tarehe ya mwisho imeekwa kwa kikosi cha usalama kutumwa Haiti.

Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha mwaka 2004/2017 – MINUSTAH, kwa ajili ya Haiti, ambacho kilikosolewa sana kilikuwa na maafisa 6,700.

Kulingana na shirika la utafiti la International crisis group, Kenya inakadhiria kwamba kikosi kwa ajili ya Haiti kinastahili kuwa na walinda usalama wasiopungua 5,000 na kitagharimu dola milioni 240 kwa mwaka.

Nani atagharamia oparesheni ya usalama Haiti?

Marekani ndio mfadhili mkubwa kwa ajili ya oparesheni usalama Haiti. Imeahidi dola milioni 200.

Marekani imesema kwamba Guyana pia imeahidi kuchangia kifedha kwenye oparesheni hiyo, lakini kiwango cha pesa hakijatangazwa.

Canada imeahidi dola milioni 59

Ufaransa imeahidi fola milioni 3 pamoja na kutoa mafunzo ya lugha kwa walinda usalama kwa gharama ya dola 924,000.

Hata hivyo, kufikia mwezi tarehe 5 March 2024, msemaji wa umoja wa mataifa alisema kwamba dola milioni 78 pekee zimeahidiwa kutolewa rasmi, huku dola milioni 11 pekee zikiwa zimepatikana, ikiwa ni mchango kutokakwa Canada na Ufaransa.

Hakuna mchango mwingine wa pesa umetolewa tangu Haiti ilipotangaza dharura ya kitaifa.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres, mara kadhaa, ametoa wito kwa nchi kujitokeza na kuchangia kifedha na vile vile nchi zinazozungumza kifaransa kujitolea kusaidia Haiti.

Ahadi zisizoeleweka, malengo yanajulikana

Nchi kadhaa zimetoa ahadi zisizokuwa rasmi kusaidia Haiti kiusalama.

Miongoni mwa nchi hizo ni Spain na Jamaica ambayo ni jirani wa Haiti.

Mongolia, Guatemala, Italy, Peru na El Salvador zilisema kwamba zitasaidia katika kutoa taarifa za kiufundi baada ya kutuma wataalam Haiti ili kujua namna ya kukabiliana na hali nchini humo. Haijabainika iwapo nchi hizo zilituma wataalam namna zilivyoahidi.

Jamhuri ya Dominica, licha ya kutaka jumuiya ya kimataifa kutuma kikosi cha usalama Haiti, imesema haitashiriki katika usalama wa jirani yake.

Rais wa Dominica vile vile amesema kwamba hatakubali wakimbizi kutoka Haiti kuvuka mpaka na kuingia nchini mwake.

Dominica, imewarudisha nyumbani maelfu ya raia wa Haiti waliokuwa wamevuka mpaka mwaka uliopita. Nchi hiyo pia hairuhusu watoto wa wakimbizi wanaozaliwa kwenye ardhi yake kupata uraia wa Dominica.

Matumizi ya nguvu

Umoja wa mataifa umeruhusu kikosi cha usalama kwa ajili ya Haiti kutumia kila mbinu muhimu dhidi ya magenge ya uhalifu.

Imetaka kikosi hicho kushirikiana na polisi wa Haiti ili kuruhusu msaada wa kibinadamu ma kuhakikisha kwamba ukandamizaji wa haki za kibinadamu unakoma.

Makundi ya uhalifu yameungana, kiongozi wao anataka kuwa rais wa Haiti

Makabiliano ya risasi yanaendelea katika mji mkuu. Kiongozi wa magenge ya uhalifu Jimmy "Barbecue" Cherizier ametangaza kwamba kundi lake la G9 limeungana na makundi mengine kumlazimisha waziri mkuu Ariel Henry kujiuzulu.

Waziri wa fedha Patrick Boivert, ambaye anashikiliwa nafasi ya waziri mkuu ametangaza amri ya kutotoka nje masaa ya jioni ili kukabiliana na hali hiyo tete.

Mnamo terehe 5, March 2024, Cherizier alionya kwamba iwapo waziri mkuu hatajiuzulu, na iwapo jumuiya y akimataifa itaendelea kuunga mkono serikali ya sasa, nchi hiyo itatumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na kwamba mauaji makubwa yatatokea.

Cherizer, ametangaza kwamba anataka kuwa rais wa Haiti.

Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Linda Thomas-Greenfield, ameambia waandishi wa habari kwamba utawala wa rais Joe Biden umemtaka Henry kuunda baraza la serikali ya mpito itakayoongoza taifa hilo kuandaa uchaguzi mkuu.

Kuna ripoti za wanasiasa wengine wa Haiti kuanza kuunda miungano ya kisiasa kwa lengo la kuongoza nchi hiyo wakati Henry yupo nje ya nchi.

Kati ya wanaounda miungano ya kisiasa ni aliyekuwa kiongozi wa waasi Guy Philippe na aliyekuwa seneta Moise Jean Charles.

Makundi ya uhalifu yanashikilia miundo msingi muhimu ya Haiti, tangu waziri mkuu Henry alipokwa Kenya.

Mbona kuna msukosuko mkubwa Haiti?

Nchi hiyo ndogo imekumbwa na migogoro ya kisiasa kwa muda wa miaka 20 sasa. Hali ya maisha ni ngumu. Ufisadi serikali ndio sababu kubwa.

Ghasia za sasa zilianza mwezi Februari baada ya Henry kuahidi kuandaa uchaguzi mkuu, lakini akasongesha tarehe ya uchaguzi hadi katikati mwa mwaka 2025.

Alitarajiwa kujiuzulu mwezi Februari lakini alikataa kufanya hiyo na hivyo kupelekea hasira kubwa kati ya raia wa Haiti na kuongezeka kwa mashambulizi kutoka kwa magenge ya uhalifu.

Kabla ya ghasia kuongezeka zaidi mwezi Februari, uhalifu ulikuwa unaongezeka tangu kuuawa kwa waziri mkuu Jovenel Moise mnamo mwaka 2021.

Moise, alikuwa anakabiliwa na hali ngumu ya uchumi na mgogoro mkubwa wa kisiasa.

Henry aliapishwa kuwa waziri mkuu, akiungwa mkono na jumuiya ya kimataifa lakini hajapata uungwaji mkono mkubwa wa watu wa Haiti kutokana na gharama ya juu ya maisha.

Haiti imeshindwa kuandaa uchaguzi mkuu kwa miaka kadhaa na kwa sasa, hakuna kiongozi aliye madarakani amechaguliwa kupitia uchaguzi mkuu.

Idadi ya makundi ya uhalifu Haiti

Kuna karibu makundi 200 ya uhalifu nchini Haiti. Makundi makubwa 23 yanaaminika kuwa katika mji mkuu wa Port-au-prince.

Kulingana na umoja wa mataifa, makundi ya uhalifu yanashikilia asilimia 80 ya mji mkuu.

Biashara haramu ya silaha na malipo kwa makundi yanayoteka nyara watu vinaripotiwa kuwa sababu kuu ya kuongezeka kwa makundi ya uhalifu.

Polisi wa Haiti hawana ufadhili wa kutosha kutekeleza majukumu yao vipasavyo.

Forum

XS
SM
MD
LG