Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 29, 2024 Local time: 08:01

Wajumbe 350 wakutana Kenya kujadili upatikanaji wa mbegu bora


Wakulima wa vitunguu mpakani mwa Senegal na Mauritania. Picha na JOHN WESSELS / AFP
Wakulima wa vitunguu mpakani mwa Senegal na Mauritania. Picha na JOHN WESSELS / AFP

Wajumbe zaidi ya 350 wa serikali, taasisi za utafiti na makampuni yanayotengeneza mbegu wanakutana Kenya wiki hii kujadili changamoto za upatikanaji wa mbegu –bora kwa ajili ya wakulima wa Kiafrika.

Wataalamu wamesema ukosefu wa mbegu bora unaathiri uzalishaji wa chakula katika bara hilo na kuchangia janga la njaa katika nchi nyingi.

Kulingana na mashirika ya Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu milioni 280 Afrika, hawana usalama wa chakula, huku zaidi ya bilioni moja wanashindwa kumudu kupata lishe bora.

Moja ya matatizo ni kwa wakulima wengi wa Afrika kushindwa kupata mbegu bora, na kusababisha kushuka kwa kiwango kikubwa cha mazao.

Mwezi Oktoba mwaka 2022, Kenya iliidhinisha matumizi ya mbegu ambazo zimefanyiwa mabadiliko ya kijenetiki baada ya marufuku ya miaka 10.

Hata hivyo, kuondolewa kwa marufuku hiyo kuliwatia hofu majirani zake ambao hawakuwa na uhakika na mbegu za GMO na bidhaa zake.

Tanzania ilisema itafuatilia katika mipaka yake kuzuia chakula chochote cha aina hiyo kutoka Kenya.

Forum

XS
SM
MD
LG