Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 03, 2024 Local time: 23:47

Wakaazi wa Niger wameandamana kupinga uwepo wa jeshi la Marekani


Ramani ya Niger ikionyesha mji mkuu wa Niamey pamoja na nchi inazopakana nazo.
Ramani ya Niger ikionyesha mji mkuu wa Niamey pamoja na nchi inazopakana nazo.

Washington  ilijenga kambi yenye thamani ya dola milioni 100 kwa ajili ya kurusha ndege zisizokuwa na rubani kutoka Niger

Mamia ya watu waliandamana leo Jumapili kupinga uwepo wa wanajeshi wa Marekani katika eneo linalotawaliwa na jeshi la Niger ambako ujumbe kutoka Washington unatarajiwa ndani ya siku kadhaa kupanga mpango wa kuondoa vikosi hivyo.

Marekani ilikubali siku ya Ijumaa kuondoa wanajeshi wake zaidi ya 1,000 kutoka taifa hilo la Afrika ambako Washington ilijenga kambi yenye thamani ya dola milioni 100 kwa ajili ya kurusha ndege zisizokuwa na rubani. Maandamano hayo katika mji wa kaskazini wa jangwa wa Agadez, makazi ya kituo cha jeshi la anga la Marekani, yaliitishwa na muungano wa kundi la vyama 24 vya kiraia ambavyo vinauunga mkono utawala huo tangu mapinduzi ya mwaka jana.

"Hii ni Agadez, sio Washington, jeshi la Marekani rudini kwenu, lilisomeka bango kubwa lililokuwa limeshikiliwa na waandamanaji". Issouf Emoud ambaye anaongoza vuguvugu la M62 mjini humo, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba "Ujumbe wetu uko wazi: Wanajeshi wa Marekani wanatakiwa kufunga virago na kurudi nyumbani".

Forum

XS
SM
MD
LG