Svoboda | Graniru | BBC Russia | Golosameriki | Facebook

Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 30, 2024 Local time: 07:46

Waziri wa ulinzi wa Marekani akutana na mwenzake wa China


Waziri wa ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin
Waziri wa ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin

Pentagon imesema Lloyd Austin na Admirali Dong Jun wa China walijadili uhusiano wa ulinzi na masuala ya usalama wa kimataifa

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alizungumza na mwenzake wa China leo Jumanne, ikiwa ni mazungumzo ya kwanza kati ya wakuu wa ulinzi wa nchi hizo mbili katika kipindi cha miezi 17.

Pentagon imesema Austin na Admirali Dong Jun wa China walijadili uhusiano wa ulinzi na masuala ya usalama wa kimataifa kutoka kwa vita vya Russia nchini Ukraine ambavyo havikuwa na uchokozi wowote na mpaka hivi karibuni uchokozi kutoka Korea Kaskazini.

Taarifa kwa vyombo vya habari imesema Austin alisisitiza umuhimu wa kuheshimu uhuru wa bahari ya juu wa usambazaji kama iuivyohakikishiwa kwenye sheria za kimataifa, hasa katika South China Sea.

Waziri wa ulinzi wa China, Dong Jun
Waziri wa ulinzi wa China, Dong Jun

Beijing imesisitiza nia yake ya kudhibiti upatikanaji wa South China Sea na kuileta Taiwan chini ya udhibiti wake, kwa nguvu ikiwa ni lazima. Wakati huo huo Rais Joe Biden amesema wanajeshi wa Marekani watakilinda kisiwa hicho kinachoendeshwa kidemokrasia dhidi ya mashambulizi.

Forum

XS
SM
MD
LG