Vikosi vya Russia, vilifyatua makombora saba kutoka mkoa wa Belgorod na Black Sea katika malengo ya Ukraine, Aprili 20, jeshi la anga la Ukraine limeripoti.
Shambulizi la anga ya Israel, kwenye nyumba moja katika mji wa kusini mwa Gaza limesababisha vifo vya watu tisa, sita kati yao wakiwa watoto, maafisa wa hospitali wamesema Jumamosi, wakati Israel ikiendelea na mashambulizi yake ya takriban miezi saba katika eneo lililozingirwa la Palestina.
Mlipuko mkubwa katika kambi ya jeshi nchini Iraq mapema Jumamosi umemuua afisa wa kikosi cha usalama cha Iraq, kinachojumuisha makundi yanayoungwa mkono na Iran.
Zaidi ya watu 2,500 wameuwawa au kujeruhiwa katika ghasia za magenge nchini Haiti kuanzia Januari hadi Machi, zikiwa zimeongezeka kwa asilimia 53 katika miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2023, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haiti (BINUH) imeeleza.
Takriban watu 1,300 wamekimbia kutoka mashariki mwa Myanmar kuelekea Thailand, maafisa wamesema Jumamosi, wakati mapigano mapya yakizuka katika mji wa mpakani ambao hivi karibuni ulitekwa na wapiganaji wa msituni wa kikabila.
Vyombo vya habari vya Marekani vimesema kuwa Israel imefanya mashambulizi ya anga nyakati za alfajiri ndani ya Iran Ijumaa vikiwanukuu maafisa wa Israel na Marekani ambao hawakutajwa majina.
Shirika la Afya Ulimwenguni limeidhinisha toleo la chanjo mpya inayotumika kwa kiasi kikubwa ya kipindu pindu
Viongozi wa Ulaya wako katika siku ya pili ya mkutano hivi leo wa Baraza la EU mjini Brussels, ambapo mazungumzo hivi leo yanalenga jinsi ya kuondoa tatizo la kushuka kwa uchumi katika umoja huo na kuuzuia kuwa nyuma zaida ya China na Marekani.
Qatar inafikiria tena jukumu lake kama mpatanishi kati ya Israel na Hamas, waziri mkuu amesema jana wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Doha akiwa na mwenzake wa uturuki.
Moscow imekwepa kulaani shambulizi la Iran dhidi ya Israel wakati ikiwataka viongozi wa Israel kujizuia.
Pentagon imesema Lloyd Austin na Admirali Dong Jun wa China walijadili uhusiano wa ulinzi na masuala ya usalama wa kimataifa
Pandisha zaidi