Radio
06:00 - 06:29
Mpango wa ICC kumfungulia Joseph Kony mashtaka kabla hajakamatwa waibua hisia mseto
Waathiriwa wa ukatili wa kundi la waasi la Lord's Resistance Army, LRA, nchini Uganda, wamekuwa na maoni mseto, kuhusu mipango ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuanzisha kesi dhidi ya kiongozi mtoro wa kundi hilo, Joseph Kony, bila kuwepo mahakamani.
19:30 - 19:59
Waziri wa mambo ya nje wa Afrika kusini anasema hataki kuzungumzia zaidi ripoti ya jopo inayomchunguza Rais Ramaphosa juu ya ufisadi wa 2020
Matokeo ya jopo hilo yanakuja chini ya mwezi mmoja kabla ya mkutano wa uchaguzi ambao utaamua ikiwa Rais Ramaphosa atawania muhula wa pili kwa tiketi ya chama cha African National Congress (ANC) katika uchaguzi wa mwaka 2024
21:00 - 21:29
Vita dhidi ya Ukimwi vinaonekana kukosa nguvu kutokana na juhudi nyingi zinazoangazia mabadiliko ya hali ya hewa na ukuaji wa uchumi
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.