Kenya imeongeza uwezo wake wa kukabiliana na ugaidi na uhalifu mwingine kama ulanguzi wa dawa za kulevya baada ya kuzindua kituo maalum kitakachofanikisha shughuli za maafisa wa polisi katika kitengo cha kukabiliana na ugaidi Pwani ya Kenya.
Zaidi ya vijana 400 wamematwa katika operesheni ya pamoja ya vyombo vya usalama katika eneo la Karamoja, huku juhudi za serikali za kuhamasisha vijana kuendelea na maosmo zikionekan kutofua dafu.
Rais wa Marekani Joe Biden amepimwa na kupatikana na virusi vya Covid-19. Kwa mujibu wa msemaji wa White House Karine Jean-Pierre, rais huyo ana dalili zisizo kali za ugonjwa huo.
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.