Radio
Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan aendelea kuwa na uhusiano wa karibu na Putin.
Tangu Erdogan aliposimamia makubaliano ya usafirishaji wa nafaka kutoka bandari za Ukraine pamoja na mauzo ya mbolea kutoka Russia., kiongozi huyo amekuwa na ushirikiano mkubwa na Putin , wakati mataifa mengine yakiendelea kumwekea vikwazo.
Tanzania Universities Abroad yasaidia vijana kupata ajira nje ya nchi.
Vijana wanaomaliza vyuo vya elimu ya juu baso wana changamoto kubwa ya kupata ajira Taasisi ya Universities Abroad inafanya juhudi za kuwapatia nafasi vijana hao wasomi na wasio na elimu ya juu katika nchi za Poland, Finland na Ujerumani.
Raia wa Angola wajiandaa kwa uchaguzi mkuu kesho
Wagombea urais nchini Angola Jumatatu walihitimisha kampeni za mwezi mzima kabla ya uchaguzi wa Jumatano ambao huenda ukashuhudia ushindani mkali kati ya chama tawala, kilicho madarakani kwa miongo kadhaa, na upinzani unaozidi kuongeza mvuto miongoni mwa vijana.
Kwa Undani: Uchaguzi Angola; Joao Lourenco anatafuta muhula wa 2, upinzani umetishia kutumia njia zote kupinga matokeo
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.