Radio
Jeshi la Somalia lasema kwamba zaidi ya vijiji 20 karibu na mpaka wa Ethiopia vimekombolewa kutoka mikononi mwa al-Shabab.
Ripoti zimeongeza kusema kwamba operesheni hiyo imewezekana kutokana na ushirikiano kati ya jeshi la raiya wenye silaha, pamoja na mashambulizi ya anga kutoka kwa taifa ambalo halijafichuliwa.
William Ruto aapishwa rais wa tano wa Kenya
William Ruto ameapishwa kama rais wa tano wa Kenya siku ya Jumanne, wiki moja baada ya Mahakama ya Juu kuidhinisha uchaguzi ambao ulikatiza matumaini ya familia mashuhuri za kisiasa nchini humo na kumpa mamlaka mtu ambaye alianza kazi yake kama muuza kuku kando ya barabara.
Rais William Ruto wa Kenya ameahidi kuendeleza ushirikiano wa ndani na washirika wa kikanda ili kuimarisha maisha ya wakenya
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Dr William Rutto ala kiapo cha kuwa Rais wa tano wa Kenya
Dr William Rutto ameapishwa kuwa rais wa tano wa Kenya, akichukuwa uongozi kutoka kwa Uhuru Kenyatta. Toka kifo cha Malkia wa Uingereza Elizabeth II, kumekuwa na mijadala na hoja mgongano juu ya nafasi ya malkia na ufalme wa Uingereza kwa bara la Afrika.