Radio
16:30 - 16:59
Vijana wa Burundi waondoka kwa wingi nchini mwao kutafuta ajira nchi za Ulaya
Vijana wengi wa Burundi wamekua wakiondoka nchini mwao na kuelekea Serbia kutafuta ajira, baada ya serikali ya Burundi na Serbia kusaini makubaliano ya kuruhusu raia wa Burundi kuingia Serbia bila visa. Lakini baadhi ya vijana hao hujipenyeza na kuingia Ubelgiji kwa kufanya safari hatarishi.
19:30 - 19:59
Mamia ya vijana wa Sudan wafunga safari kuelekea Mistri kutafuta maisha bora
Mamia ya vijana wa Sudan wanafanya safari kuekelea Mistri upande wa kaskazini ili kutafuta maisha bora, kutokana na matatizo ya kiuchumi na kisiasa nchini mwao. Umoja wa mataifa unasema hali hii inasababishwa na ukosefu wa chakula na ajira nchini Sudan.
21:00 - 21:29
Kwa Undani: Putin anatuma wanajeshi 300,000 Ukraine, Umoja wa ulaya umesema vita vimefikia kiwango cha hatari kubwa
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.