Wito huo umetolewa wakati shinikizo likitolewa kwa wanawake kushiriki vilivyo katika kuwania nafasi za kisiasa wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka ujao.
Wanafunzi 25 kutoka jamii ya wafugaji ya kabila la Wamasai jijini Arusha waliokuwa wafanyiwe ukeketaji ikiwa ni maandalizi ya kuozeshwa, wamenusurika kufanyiwa kitendo hicho. Vijana waaswa kuzungumza yanayowasibu ili kuepusha vishawishi vya kujiua.
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
Kwa Undani ni matangazo ya dakika 25 yanayochambua habari kwa undani zaidi na kumpa msikilizaji maelezo ya kina kuliko ilivyo kawaida kuhusu tukio au swala lililojitokeza katika habari.